Diamond Hakumwacha Tanasha, Tanasha Ndio Kamwacha Diamond Baada ya Kupigwa Matukio



Baada ya Tanasha na Simba kutemana, Tunda wa katibu la umbea akiwa katika mahojiano naBongo Tosh alizungumzia mambo kadhaa kuhusu uhusiano wa Diamond na mpenziwe Tanasha.


Hii ni baada ya Tanasha kukusanya virago vyake na kurudi humu nchini, alifanya kitendo hicho alipokatazwa kuenda hafla moja nche ya nchi.

Tunda alikuwa na haya ya kusema,

“Tanasha anapost vitu ambavyo anapost kwa maana ameumia sana anajaribu kutoa maumivu moyoni mwake anaelezea kilicho moyoni mwake kupitia post hizo

Kwa kusema ukweli Tanasha hakuwa na upendo kamilifu kwa Simba alikuja tu kama wasanii wale wengine ili akuze kipaji chake cha uimbaji

Kwanini nasema Tanasha kaacha Diamond hii ni kwa sababu yeye mwenyewe ndio alijiondoa nyumbani na kuenda hakufurushwa na mtu yeyote.” Alieleza Tunda.


Tanasha kutema Simba kulitokea wakati alipost ujumbe kwenye mtandao wake wa kijamii wa Instagram, akisema kuwa Diamond hana heshima na aaminiki kwa chochote.

“Wacha nisema Tanasha alikuwa amekuja kwa Diamond kwa lengo lake alipitia kwa nia ya kimapenzi kukuza muziki, alijisongeza karibu na Diamond ili awe akienda na Diamond kila mahali

Alikuwa anataka aende na yeye ili ajulikane kwenye mataifa yote, ilhali hajasainiwa na lebo la WCB, kitu ambacho mameneja hawajakubaliana nacho.” Alieleza Tunda.

Alisema kuwa Tanasha hakufurahishwa na kuachwa na Diamond alipokuwa anaenda katika tour yake ya muziki.


“Hakufurahishwa kabisa, lakini sababu za wimbo wa Diamond na Tanasha kutowekwa katika kurasa za Tanasha

Ni kwa sababu meneja wa WCB washaajua lengo la Tanasha kuwa na Diamond, mzazi ni mzazi lazima asimame katika lengo lake hata kama uwe nani.” Alieleza Tunda.

Kufikia sasa msanii maarufu wa nyimbo za bongoDiamond almaarufu Simba hajaweza kuzungumza chochote kuhusiana na tukio hilo alilolifanya Tanasha.

Photo Credits: radiojambo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad