"Napenda Wanawake Wenye Vipato" - Dulla Makabila Afunguka Kuhusu Kuwa Marioo Mpenda Vitonga



Msanii wa muziki wa singeli Dulla Makabila, amefunguka na kusema yeye sio marioo wala king'asti ila huwa anapata bahati ya kupendwa na wanawake ambao wanavipato vikubwa.


Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, Dulla Makabila amesema binafsi hapendi wanawake wasio na vipato kwa sababu yeye mwenyewe bado anatafuta pesa.

"Mimi sio mtu wa dizaini ya marioo au king'asti, natafuta pesa zangu mwenyewe, ila ni mtu ambaye nina bahati ya kupendwa na wanawake ambao wapo vizuri kimaisha na wenye pesa sio kwamba ndiyo ninaowatafuta, kwa sababu sisi wanaume kuigiza hatujui kama unampenda  mwanamke kwa ajili ya pesa zake atajua tu" Dulla Makabila.

Aidha msanii huyo ameongeza kwa kusema "Pia ninampenda mwanamke mwenye kipato na hata asingekuwa na kipato bado ningempenda tu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad