Facts Muhimu kuhusu WCB "Harmonize Usajili Bora zaidi Aliyowahi Kufanya Diamond, Rayvanny Akitoka WCB Miezi Sita tu Chali..


1. Kuna wanaolalamika eti madogo pale WCB wanalaliwa na Mondi, naomba mjue kwamba WCB ni biashara ya Mondi so yupo pale kumake hela kupitia akina Rayvanny, Mbosso, Lavalava, Tale, Sallam, Laizer n.k, kwa maana nyingine WCB ni mali ya Mondi so ndo kitega uchumi chake kile.

2. Watu wanamsema Harmonize kwamba ameishiwa, kufikisha views 1m you tube imekuwa mbinde, ambacho hukijui ni kwamba ukiwa Wasafi automatic mashabiki wa Mondi wote ni wa kwako, so wanaokushabikia sio kweli kwamba ni mashabiki wako pekee wapo pia wa Mondi na WCB kiujumla, so unapotoka WCB sasa ndo unaanza kutengeneza mashabiki wako, na automatic mashabiki wa Mondi na WCB watakuwa against wewe, ndo kipindi ambacho anapitia Harmonize, hata hivyo bado anajitahid sana, Kumbuka Mavoko baada ya kutoka kilitokea nini? Itakuwaje siku akiaamua kutoka Lavalava nadhani itabidi akafanye kilimo tu.

3. Diamond platnumz ni mjanja sana na tayari amefikia level ya kutoshuka tena labda aamue tu kuacha mziki na bado atakapoamua kurudi atatikisa tena, ni kama Mzee Yusuph kwenye taarabu, tangu aache taarabu pengo lake linaonekana na mziki wa taarabu unammiss siku atajayeamua kurud ataanzia pale alipoishia kwenda juu kamwe hawezi kuwa chini ya pale.

4. Harmonize, Yes huyu jamaa ndo definition halisi ya kijana mpambanaji, dogo alijipanga muda mrefu sana kufanya kitu chake tangu akiwa ndani ya WCB, pale Wasafi ni kama alikuwa shuleni na ile kupata bahati ya kuwa karibu na Mondi ni kama alipata nafasi ya kuwa karibu na El chapo na huku ukiwa na ndoto ya biashara ya mihadarati, unachokifanya ni kuandaa note book kubwa na kuandika kila kitu, then baadae unajisomea na kufanya utekelezaji

5. Diamond anammiss Harmonize, hakuna msanii kama Harmonize Wasafi, ule ndo ulikuwa usajili bora na nachelea kusema unaweza ndo ukawa usajili bora zaidi kt historia ya Wasafi, Nyimbo alizoimba Mondi na Harmo zimesafiri umbali mrefu sana kuliko collable yoyote east africa, Harmo alimbeba Mondi ndani yake, alipokuwepo Harmo hapakuwa na sababu sana Mondi awepo.

6. Rayvanny, This guy is multi-talented hakuna ubishi juu ya hilo, anaimba, anatunga, anarap, ana vocal kali sana lakin kuna kitu anakosa, Focus... katika miaka hii michache ni kama tayari amemaliza kutoa kila kitu alichokuwa nacho, anaimba muziki ambao ukiusikia utakimbilia kuudownload lakin kesho jioni ndo utakuwa wa kwanza kuufuta, amelimbilia kujijenga kibiashara zaidi kabla ya kujijenga kimuziki.

Hapa ndo Mond anapowin, kabla ya kuubadilisha muziki kuwa biashara na kuleta janja janja zake alianza kwa kufanya muziki kwanza, watu wakapenda muziki wake then alipoanza kuleta ujanja ujanja tayari alikuwa na mashabiki wengi so si rahisi kumkimbia tena, unataka kujua utofauti wa muziki mzuri na muziki biashara kwa mondi simple nenda kasikilize Mbagala, Moyo wangu, Nitarejea, utanipendaga na uje usikilize Baba lao, Jeje n.k. Harmo amelielewa hilo ndo maana kwenye album yake kuna muziki mzuri kwa wingi kuliko muziki biashara, jamaa amepata kitu kwa Mondi, tena sana, Rayvanny akitoka wasafi leo baada ya miezi 6 mtamkuta Tukuyu analima mpunga

7. Lazima ujue WCB kwasasa ni bonge la Platform, mtu yoyote akiwa pale ataonekana na kusikika, unadhan Lavalava ana ukali sana kuliko Jux, Ben pol, Marioo.. lakin dogo anasikika sana eti, Ni Wasafi hiyo inawabeba

8. Mbosso, Yes huyu dogo ana kitu, hataki janja janja yeye anataka kufanya mziki, baada ya miaka mitano huyu dogo tumuangalie mwa jicho la 3 anaweza kufika mbali, japo mziki wake ni kama anatarget sana wanawake lakin ana kitu fulan kipo, na mimi nadhan bado Mbosso ana kitu zaidi tunamdai, hajatupatia bado.. ila kitendo cha kuwa Wasafi ambayo ni biashara ya Mondi anaweza akajikuta anabanwa na kutotoa baadhi ya vitu, lakin Yes mbosso tuendelee kumtazama..

Naomba niishie hapo.....

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad