Fahamu Makosa na Faini za Viongozi wa Chadema



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu Viongozi wakuu wa CHADEMA na mmoja aliyehamia CCM Vicent Mashinji kulipa faini kwa mashitaka 12 kati ya 13 yaliyokuwa yakiwakabili wakati shitaka moja la kupanga njama likiondolewa na Mahakama.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Thomas Simba leo Machi 10, 2020, ametoa hukumu kwa Mbunge wa Hai kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, kulipa faini ya shilingi milioni 70.

Mahakama hiyo imetoa hukumu kwa John Mnyika, Salum Mwalimu, Easter Matiko na Vicent Mashinji kila mmoja kulipa faini ya Shs Milioni 30. John Heche, Msigwa, Mdee na Bulaya Milioni 40 huku.

Mbowe na viongozi wenzake saba pamoja na aliyewhi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt Vicent Mashinji, wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo ya uchaguzi.

Katika shtaka la pili kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh10 milioni au kwenda jela miezi mitano (5).

Shtaka la 3 hadi 6, kila mshtakiwa atalipa faini ya Sh10 milioni au jela miezi mitano. Hata hivyo shtaka la 9, 10 linamhusu Mbowe peke yake hivyo kila kosa atalipa Sh5 milioni au jela miezi mitano.

Na shtaka la 11 atalipa faini ya Sh10 milioni. Mbowe ametiwa hatiani katika mashtaka manane, ambayo ni shtaka la 2, 3, 4, 5, 6, 9, 10 na 11.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad