Fatma Karume amcharua Makonda kutangaza mtoto wa Mbowe ana Corona



Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amemcharua Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kitendo cha kumtangaza mtoto wa Freeman Mbowe kuwa ni mgonjwa wa Corona.

“@makonda-paul huna mamlaka ya kumtaja mgonjwa kwa jina,” aliandika Fatma Karume katika ukurasa wake wa twitter.

Aliongezea kuwa “Ilikuwa upeleke Ambulance kwenda kumchukua awekwe Quarantine na si kumtaja hadharani,” aliandika.

Fatma aliandika ujumbe huo baada ya kuona Makonda anamjibu Waziri wa afya jamii na maendeleo, jinsia, wazee na watoto kwa kudai yupo sahihi kwa asilimia 100 kutangaza kwa kuwa ni mwenyekiti wa usalama mkoa wa Dar es salaam

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyunae Kazukia wapi??
    Wakili wa kujitegea!!???
    Hiyo leseni kaipata wapi?? na Lini imetoka na inakwiisha lini..muwe makini ndugu zangu mkiandika Credentials is necessary . huyu hana hizo siffa. Labda zama zile kamelius.

    Mh Makonda was right in his capacity na baada ya taarifa Dudley dokta na Mb ndiyo waseka na wao wamejikalantine.
    na kabla was businessas usual .

    Well done Makonda..!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad