Halima Mdee "Wabunge Wote Tupimwe Corona"



Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima James Mdee, leo katika kikao cha kwanza cha mkutano wa kumi na tisa wa bunge ametoa ombi kwa serikali, wabunge wote wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania kupimwa ili waweze kushiriki vikao vya bunge.

Amezungumza hayo alipopata nafasi ya kuuliza swali kwaajili ya ufafanuzi baada ya taarifa iliyotolewa na Spika wa bunge, Job Ndugai juu ya utaratibu mpya wa vikao vya bunge utakavyokuwa ili kukinga maambukizi ya virusi vya covid 19 kwa wabunge.

“leo wabunge wapo kwenye vyumba (utaratibu mpya wanaoingia bungeni ni 150 kati ya wabunge zaidi ya 300) kwanini tusianze na sisi tupimwe wote tukijijua tupo salama tukae hapa tu ‘debate’, hili ndio bunge la mwisho mh. kuelekea uchaguzi mkuu” Amesema Mdee.

 Aidha Spika Ndugai amesema kuwa wazo hilo ni zuri na litafikiriwa jinsi ya kulifanyia kazi, huku awali wakati akitoa taarifa yake amesema wabunge ambao hawatapata nafasi ya kuingia bungeni watafuatilia shughuli za bunge kupitia runinga katika kumbi na maeneo mengine yaliyopangwa.

Sambamba na hayo Ndugai amesema tahadhari zinazoendelea kuchukuliwa katika nchi yetu kukinga maambukizi ya virusi vya Covid 19 hatizaweza kuendana moja kwa moja na zile za nchi nyingize zilizoendelea kwani watanzania wana mfumo tofauti wa maisha.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wazo ni Zuri.
    Je unataka kuthibitisha kwa Thermal camera Detectors Hazifanyi kazi au hazijakuwa installed gateni..??

    As this, is a Mandatory requirement.

    If not,We need to Act and install NOW.

    ReplyDelete
  2. Wazo ni Zuri, na Wakati ni Muafaka.

    Je unataka kusema kuwa Thermal Detectors Camera's Hazifanyi kazi, au hazijakuwa installed getini..??

    As this, is a Mandatory requirement.

    If not,We need to Act and install NOW.

    ReplyDelete
  3. Kwa Mara ya Kwanza katika kipindi chaUwakilishi wa miaka mitano Halima ameweza kuzungumza kiu hiki which bring s sense in a sensible way.

    HongeaHalima kwa mara ya kwanza kongea kitu cha maana. wakati wa lala Salama.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad