DAR: Baada ya wimbo wake wa Singeli wa Hujanikomoa kufanya vizuri kimataifa, staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’ amefunguka kuwa muziki huo ni tundu lingine la kutoboa kimaisha.
Harmonize au Harmo aliliambia Gazeti la IJUMAA kuwa, atafanya kila awezalo kuhakikisha muziki huo unatoboa kimataifa kwani tayari umeonesha mwanga.
Wimbo huo wa Harmo, bado ‘unatrendi’ na kufanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga.
Staa huyo amewataka wasanii wenzake kuchangamkia fursa hiyo kama ilivyokuwa kwa Bongo Fleva.
“Hii ni fursa nyingine ambayo tunapaswa kuiona na kuichangamkia,” alisema Harmo ambaye Machi 14, mwaka huu atazindua albam yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Afro Beat kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar.
Stori: NEEMA ADRIAN, Ijumaa