Takwimu za kuwa mtu gani tajiri duniani zinatolewa na majarida mbalimbali kwa sasa duniani lakini jarida la Forbes ndio ambalo linaaminika sana ambalo lilimtaja Jeff Bezos ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Amazon likimueleza kuwa ndiye mtu tajiri zaidi duniani kwa sasa ambapo walitoa orodha hii ya mwaka 2019, Jarida hilo la Forbes likiutaja utajiri wake kuwa ni ni TZS 300.1 trilioni ambazo ni sawa na ($131 bilioni).
Licha ya utajri huo wa Bezos lakini imeelezwa kuwa sio mtu tajiri zaidi kuwahi kuishi duniani, na kwamba anayeshika nafasi hiyo ni mtu mmoja aliyewahi kuwa kiongozi wa taifa la Mali katika karne ya 14, Mansa Musa. Kiongozi huyu alikuwa ni tajiri kiasi kwamba ni vigumu kujua kwa uhakika thamani ya utajiri wake ilikuwa ni shilingi ngapi.
Mwaka 2015 tovuti ya money.com ilisema kuwa Mansa Musa alikuwa tajiri kuliko inavyoweza kuelezwa.
Mwaka 2012 tovuti moja ya nchini marekani, Celebrity Net Worth ilisema kuwa utajiri wa kiongozi huyo ulikuwa ni TZS 917 trilioni, lakini wana historia wanasema kuwa ni vigumu kuuweka utajiri wake katika namba.
Kwa mujibu wa majarida mawili makubwa ambayo ni Money.com, Celebrity Net Worth, Hapa chini ni orodha ya watu 10 matajiri zaidi kuwahi kuishi duniani :
Mansa Musa (1280-1337) Mfalme wa Mali. Utajiri wake hauthaminiki.
Augustus Caesar (63 BC-14 AD, Mtawala wa Roman): $4.6 trilioni
Zhao Xu (1048-1085,) Utajiri wake hauhesabiki
Akbar I (1542-1605, Mtawala wa Ukoo wa Mughal kutoka India). Utajiri wake hauhesabiki
Andrew Carnegie (1835-1919, Mmilikiwa viwanda mwenye asili ya Scotland ila aliishi Marekani) $372 bilioni
John D Rockefeller (1839-1937) Mfanyabiasha wa Marekani) $341 bilioni
Nikolai Alexandrovich Romanov (1868-1918, Mtawala kutoka Urusi) $300 bilioni
Mir Osman Ali Khan ( 1886-1967, Indian royal) $230 bilioni
William The Conqueror (1028-1087) $229.5 bilioni
Muammar Gaddafi (1942-2011, Rais wa Libya) $200 bilioni