Idadi walioambukizwa virusi vya corona yaongezeka Rwanda




Wizara ya afya nchini Rwanda imesema kuwa watu wengine wawili wamepatikana na virusi vya corona.

Visa vya hivi karibuni vinaifanya Rwanda kuwa na jumla ya visa saba vya coronavirus, idadi ambayo ni kubwa zaidi kuliko iliyotangazwa katika mataifa ya jirani ya Afrika Mashariki.

Wizara ya afya nchini humo inasema kuwa watu walioambukizwa coronavirus ni: Mwanamke mmoja mwanamke mmoja Mnyarwanda aliyeolewa na Mnyarwanda mwenzake ambaye aligua baada ya kutembea katika nchi za Fiji, Marekani na Qatar''

Mwingine ni Mjerumani mwenye umri wa miaka 61 aliyewasili Rwanda tarehe 13/03 akitokea Ujerumani kupitia Uturuki, ambaye alifika Rwanda akiwa na kikohozi na kupelekwa hospitalini Machi 15.

Watu waliotangamana na watu hao wanatafutwa ili wapimwe, imesema wizara hiyo.

Serikali ya Rwanda ilitangaza kuchukua hatua kadhaa za dharura kukabiliana na janga la coronavirus, saa kadhaa baada ya kutangaza kwamba raia mmoja wa India aliyewasili nchini humo Machi 8, kuthibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Katika mahojiano na Radio Rwanda, Mawaziri Anastase Shyaka wa mambo ya ndani na Dr Ngamije Daniel wa Afya, walisema kuwa hatua hizo ni pamoja na kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.

Bwana Shyaka alisema pia kwamba makasisi wanaelewa ukubwa wa janga hili ambalo Rwanda na dunia nzima inakabiliana nalo.

Miongoni mwa hatua hizo, Bwana Shyaka alisema kwamba matukio kama vile mikusanyiko ya watu katika maeneo ya michezo na harusini ambayo yameahirishwa na kwamba wale waliopoteza wapendwa wao watazikwa kwa namna ya kipekee.

Shirikisho la Sola la Rwanda(FERWAFA), pia limetangaza kwamba michuano yote kwa sasa itafanyika bila kuhudhuriwa na mashabiki katika viwanja vya michezo, huku shirikisho la mpira wa mkono nchini humo likiahirisha michezo yake yote.

Wizara ya afya inasema muda wa kufunga shule na makanisa wa wiki mbili uliotangazwa unaweza kuongezwa zaidi kutokana na kasi ya maambukizi ya coronavirus nchini humo.

Waziri Shyaka pia alitoa wito kwa raia kuepuka mikusanyiko katika maeneo ya migahawani na masokoni.

Katika usafiri wa umaa, waziri Shyaka amesema kwamba hakuna abiria atakayeruhusiwa kusimama na kutoa wito kwa watu wa eneo na vikosi vya usalama kusaidia kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa.

Hii ni kwasababu katika maeneo ya ufasiri wa umma mfano mjini Kigali, huwa na mikusanyiko mikubwa na kuhakisha kila abiria amepata kemikali ya kuosha mikono inayoua viini kabla ya kupanda kwenye usafiri, kwa mujibu wa bodi inayodhibiti usafiri.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad