Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo leo imeripoti kifo cha kwanza kutokana na virusi vya corona pamoja na visa vitano vipya vya maambukizi.Kupitia mtandao wa twitter, waziri wa afya nchini humo Eteni Longondo, amethibitisha kifo hicho kilichotokea hapo jana pamoja na visa hivyo vipya akisema wote walioathirika ni raia wa Congo na kwamba maafisa wake wanawashughulikia.
Nchi hiyo imeripoti visa 23 kwa jumla tangu Machi 10 na kifo hicho kinaongeza idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivyo katika eneo la jangwa la Sahara barani Afrika kufikia watu watatu baada ya vifo vilivyoripotiwa wiki hii katika nchi za Burkina Faso na Gabon.
Hapo jana, serikali ya Congo, iliratibu mikakati ya kinga hasa katika mji mkuu Kinshasa ambao ni makazi ya takriban watu milioni 10 na ambapo ndiko kwenye visa vingi vya virusi hivyo kwa sasa.