Juventus yafunga kambi zote za mazoezi, watatu wabainika kuwa na Coronavirus
0
March 02, 2020
Klabu ya Juventus imevunjilia mbali kambi zote za mazoezi pamoja na kuamuru timu yao ya vijana walio na umri chini ya miaka 23 kubaki nyumbani kufuatia hofu ya Virusi vya Corona.
Vibibi kizee hivyo vya Turin, vimetangaza maamuzi hayo baada ya timu yao ya vijana ‘U23’ kucheza mechi na klabu ya US Pianese ambayo imebainika wachezaji wao watatu kuwa na viashria vya Virusi vya Corona.
Katika mchezo huo wa Serie C, kikosi cha Juventus ‘U23’ kiliibuka na ushindi wa goli 1 – 0 mbele ya Pianese ambayo wachezaji wake watatu pamoja na kocha wao kubainika kuwa waathirika.
Juve imekitaka kikosi kizima cha ‘Under-23’ kusalia nyumbani hadi ifikapo Machi 8, huku taarifa nzuri zaidi ni kuwa hakuna mchezaji yoyote anayeonesha kuwa na dalili za ugonjwa huo hatari.
Wakati kwa timu ya Juventus marufuku hiyo itaendelea kudumu mpaka pale watakapo pata taarifa ya ratiba ya mechi yao dhidi ya Inter Milan ‘game’ ya Serie A baada mchezo huo kusimamishwa kufuatia hofu ya mlipuko wa ugonjwa huo.
Hakuna mchezaji yoyote aliyebainika kuwa kuwa ameathirika licha ya kughairishwa kwa mchezo huo dhidi ya Inter Milan.
Taarifa za ndani ya Turin club zinadai kuwa hali hiyo imechukuliwa kwa umakini mkubwa sana, na madaktari wa timu wamewataka wachezaji wote kuosha mikono yao na kutumia ‘gels’.
HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>
Idadi ya waliobainika kuwa wameathirika na Virusi vya Corona nchini Italia vinafikia watu 1,049 huku vifo vikiripotiwa kuwa 29. Na taarifa za mwisho zilizotolewa na Serikali ya Italia idadi inafikia 1,128.
Tags