Kagera: Dereva wa Lori Aingia na Corona Tanzania


Miongoni mwa waathirika 13 wa virusi vya Corona nchini ambao wametajwa na Wizara ya afya, ni dereva wa lori ambaye ni mkazi wa Kagera, aliingia nchini kupitia mpaka wa kabanga kati ya Tanzania na burundi.

Akitoa taarifa ya hali ilivyo kwa sasa juu ya maambukizi ya virusi vya covid 19, waziri wa Afya, Ummy Mwalimu leo Machi 26 jijini Dodoma amesema hadi sasa Tanzania bado haina maambukizi ya ndani ‘Local transimition’ na walioathirika raia wa kigeni ni watano na watanzania 8.

” Wote hawa walipitia uwanja wa ndege wa Julius Nyerere na uwanja wa KIA,lakini huyu wa kagera ni dereva wa malori makubwa aliingia nchini kupitia mpaka wa kabanga ambao ni kati ya Tanzania na Burundi, anaendesha magari kati ya DRC, Burundi na Tanzania”

Ametaja mikoa ambayo inawagonjwa ni Arusha wagonjwa wawili, Dar es salaam wagonjwa nane, Zanzibar wawili na Kagera mtu mmoja, ambao wote walisafiri nje ya nchi na ni mmoja ambaye hakusafiri nje lakini alikutana na mtu aliyekuwa amesafiri nje ya nchi.

Aidha amesema baada ya kujiridhisha na vipimo vya sampuli za mgonjwa wa kwanza, Isabella anaandaliwa kwaajili ya kurejea kwao kwani amepona ugonjwa huo na ametoa wito kwa jamii kuto mnyanyapaa na kumnyoshea vidole.

Kwa abiria wote waliowasili nchini kuanzia tarehe 23 mwezi huu wametengwa kwenye hoteli zilizoandaliwa ambao hadi kufika jana usiku walikuwa 111 tanzania bara na Zanzibar ni watu 134.

Hata hivyo ameendelea kusisitiza kuwa wasafiri hao sio wagonjwa na wemewekwa karantini kwasababu wametoka katika nchi ambazo zimeathirika zaidi hivyo wakuu wa mikoa wanatakiwa kuhakikisha sehemu wanazowatafutia zina gharama wanazoweza kuzimudu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad