Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amelihutubia taifa lake na kutangaza mikakati mipya ikiwa ni pamoja na marufuku ya mikusanyiko ya watu zaidi ya wawili.
Hata hivyo marufuku hii haihusishi familia ama watu wanaoishi pamoja.
Baadhi ya marufuku zilizotolewa ni kufungwa kwa migahawa na huduma kama vile za ususi.
Kwa upande wa umma, watu wasioishi pamoja lazima wadumishe umbali wa mita 1.50 kati yao, Kampuni lazima zifuate kanuni za usafi kwa wafanyikazi, Kusafiri kwenda kazini, kusaidia wengine na mazoezi ya kibinafsi bado inaruhusiwa.
Sheria hizi zitatumika kwanza kwa muda wa wiki mbili. Merkel ameonya kuwa hatua hizi mpya sio mapendekezo bali ni sheria na kwamba polisi itasaidia kuhakikisha zinadumishwa.
Baada ya kutangaza sheria hizo mpya, Merkel alifahamishwa kuwa daktari aliyekutana naye siku ya Ijumaa, amegunduliwa kuwa na maambukizi ya virusi vya corona na kwamba kiongozi huyo atalazimika kuwa chini ya karantini.