Kenya yatamba mbio za kilomita 42, Kilimanjaro Marathoni



By Imani Makongoro
Kilimanjaro. Wanariadha wa Kenya wamejibu mapigo kwa kutwaa medali za dhahabi katika mbio za kilomita 42 za mashindano Kilimanjaro Marathoni yanayoendelea kwenye uwanja wa Ushirika mjini Moshi.

Lyidia Wafula alitwaa ubingwa upande wa wanawake akitumia saa 2.47.05 wakati Kiplagat Kiplimo akitaka upande wa wanaume akitumia saa 02.16.56.
Mwanariadha wa Tanzania, Sarah Ramadhan alishindwa kutamba na kuambulia nafasi ya sita, huku Failuna akijitoa kushiriki dakika za mwishoni kutokana na kupata mualiko wa kushiriki mbio nyingine za kimataifa hivi kimataifa.

Angel John ndiye Mtanzania aliyefanya vizuri katika marathoni ambapo alimaliza wa tano kwa wanawake akitumia saa 03.00.33.

Awali, Watanzania Joseph Panga na Magdalena Shauri waliibuka vinara kwenye mbio za nusu marathoni kwa wanaume na wanawake.

Watanzania saba waingia top 10, Kili mararthoni
Licha ya kutwaa medali za dhahabu kwa wanaume na wanawake, Tanzania imeweka rekodi ya kuingiza wanariadha 7 katika kumi bora (Top 10) kwa wanaume huku upande wa wanawake watano wakiingia.

Joseph Panga ndiye kinara wa wanaume akifuatiwa na Josephat Joshua huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Vicent Kimutai Towett wa Kenya.

HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Watanzania wengine walioingia katika 10 bora ni Joseph Elisante (5), Francis Damiano (6), Sylvester Naali (8), Michael Kishiba na Yohana Sulle waliomaliza katika nafasi ya 9 na 10.

Upande wa wanawake, licha ya Magdalena Shauri kuibuka kidedea, Masyelina Mbua, Neema Msuadi, Sarah Hiiti na Catheline Lange waliingia 10 bora sanjari na Wakenya watano.

Mwananchi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad