Kinara wa usambazaji, uingizaji Mirungi anaswa



Jeshi la Polisi jijini Mwanza, limefanikiwa kumtia mbaroni kinara wa usafirishaji na muuzaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi, Peter Charles Mwita alimaaarufu Peter Mirungi (46) mkazi wa Mtaa wa Rufiji, kwa makosa ya kusafirisha, kusambaza na kuuza mirungi jijini Mwanza.

Mbali na Peter jeshi hilo linawashilia watu wengine wawili kwa tuhuma za namna hiyo huku mmoja akiwakimbia polisi baada ya kuruka kutoka ndani ya gari alilokuwa akiliendesha kwenye kizuizi cha Ngashe Kata ya Lugeye, wilayani Magu.
 Mtuhumiwa huyo  ambaye  amelisumbua jeshi hilo ka miaka mingi baada ya kubaini  anafuatiliwa na polisi, Februari 1, mwaka huu alitelekeza gari lake namba T.787 DQX aina ya Probox eneo la Igoma Mashariki, likiwa na mirungi  kg 9.02.
Pia Februari  15, Peter ambaye amekuwa akifanya biashara hiyo haramu kwa muda mrefu baada ya kuwakimbia polisi aliangukia na mkono wa dola.

Aidha Machi 2, mwaka huu majira ya  12:00 asubuhi huko kwenye kizuizi cha magari kilichopo Katika Kijiji cha Ngashe, Kata ya Lugeye, wilayani Magu, askari wa doria walikamata bhangi kg 50, zikiwa kwenye magunia matatu,  ndani ya gari lenye namba za usajili T.881 AFX na tela namba T.822 CZZ Lori aina ya scania.

Gari hilo lilikuwa likitokea Tarime kuja jijini Mwanza, likiendeshwa na dereva aliyetambulika kwa jina la Joseph Achiyo ambaye aliruka kwenye gari na kukimbia baada ya kusimamishwa na askari. 28

Pia Faustine Koroso (46) mkazi wa Nyakato Mashariki na Gidion Paul (28) mkazi wa Igoma walikamatwa na polisi eneo la Nyakato Sokoni Machi 2, mwaka huu majira ya 12:30 jioni wakisafirisha mirungi kg 20  kwa kutumia pikipiki aina ya HONLG yenye namba za usajili MC 931CKL.

Kwa mujibu wa Muliro polisi wanaendelea na mahojiano dhidi ya watuhumiwa wote baada ya kukamilika kwa uchunguzi watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na kufikishwa katika vyombo sheria.

Pia amewaonya waendesha pikipiki za bodaboda wanaojihusisha na usafirishaji wa madawa ya kulevya kuwa wanachafua taswira ya biashara yao na wasithubutu kujiingiza kwenye mfumo huo.

“Sheria inazuia kulima, kusafirisha, kuuza na kutumia bangi na mirungi, ni makosa ya jinai vilevile Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawataka askari wake kufanya kazi kwa weledi na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi,”alisema Muliro.

Kamada wa Polisi mkoani Mwanza akionyesha gari lenye namba T 787 DQX mali ya Peter Charles maarufu Peter Mirungi baada ya kulikamata likiwa na kg 9.2 za dawa za kulevya aina ya mirungi. Picha na Baltazar Mashaka

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad