Mbunge wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Godbless Lema, amesema kuwa Wabunge Ester Bulaya, Halima Mdee na Jesca Kishoa hali zao bado ni mbaya na kwamba wako chini ya uangalizi wa Daktari.
Lema ameyabainisha hayo leo Machi 15, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kusema kuwa ameshangazwa kusikia kauli ya Kamanda Mambosasa, kwamba wabunge hao walienda kufanya vurugu kitu ambacho si kweli na maumivu yote wanayoyapitia kwa sasa wamesababishiwa kwa makusudi kabisa.
"Niombe uwatembelee wana hali mbaya sana, Uti wa Mgongo ni mahali sensitive, ukiniambia mimi yule aliyenyongwa mkono na hawa wengine, hawa wawili wanahali mbaya, kwa sababu Ester hata jana alikuwa anaongea kwa shida, Jesca alikuwa hawezi kuongea kabisa na ametoka kujifungua kwa upasuaji siku za hivi karibuni" amesema Lema.