Leo Nataka Kuongelea Kuhusu Huyu Mdudu Anayeitwa Corona...Je Tumekosea Wapi?


UKIONA UGONJWA UNAUA WATU WOTE BILA KUJALI WALIOOKOKA NA AMBAO HAWAJAOKOKA, BASI FAHAMU KUWA HASIRA YA MUNGU IMESHUKA KWA WANADAMU HIVYO TUNAHITAJI KUANGALIA TULIPOKOSEA NA KUTUBU.

LEO NATAKA KUONGELEA JUU YA HUYU MDUDU ANAYEITWA " KORONA"

A. KWANINI MDUDU HUYU ANAITWA KORONA?
Ugonjwa huu unaitwa KORONA kwasababu akipimwa kwa kutumia MAIKROSKOPU YA UMEME(Electronic Microscope) huyu mdudu anaonekana kama vile amevaa kofia au taji. Na sasa KOFIA kwa KILATINI inaitwa, "KORONA."
Mdudu huyu aligunduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1960 huko China.

B. JE ALITOKA WAPI KUJA KWA WANADAMU?
Huyu mdudu aliingia kwa wanadamu kupitia NGAMIA(CAMEL) na POPO(BATS). Unajua tunaposema hawa wadudu wa Korona wametoka kwa hawa wanyama wengi wanajiuliza hawa wadudu uingiaje kwa watu?

Ngoja nikueleze, virusi ni jamii ya wadudu walioumbwa na Mungu kama viumbe vingine. Na lazima ujue kila kiumbe kina sehemu yake ya kuishi. Kwa mfano, samaki anaishi baharini, ziwani na kwenye mito. Na samaki ukimwondoa kwenye maji hawezi kuishi. Vilevile na hivi VIRUS VYA CORONA makazi yake ni katika mwili wa NGAMIA na POPO.

Ngoja nikupe mfano mwingine, je unajua ugonjwa wa KISONONO? Je una habari kuwa wadudu wake walitoka katika mbwa? Mtu alifanya ngono na mbwa alileta virusi hivi kwetu.

Virusi hivi kwa mara yakwanza viligundulika mwaka 1960 katika mwili wa ngamia na popo. Kwa wakati huu vimegundulika katika mji wa WAHAN nchini CHINA mnamo 31 Dec.2019.

SWALI NI JE MDUDU HUYU ALIINGIAJE KWA WATU?

Aliingia kupitia nyama ya popo, na nyama ya ngamia na maziwa yake. Ndiyo maana hata ugonjwa wa SARS ulipoingia watu walihamasishwa kuchemsha vizuri maziwa ya ngamia na kupika nyama ya popo na ngamia hadi iive sana ili kuzuia wadudu kupenya katika mwili wa binadamu kupitia chakula. Kwa mtazamo wangu naona pia kwa kutokuwa na kiasi na tukawa walafi wa kutaka kula kila kitu madhara yake ndiyo haya sasa.

C. JE TUNAAMBUKIZWAJE NA HUYU MDUDU?

Huyu mdudu anaambukizwa miongoni mwetu kwa njia ya hewa. Mtu anapopiga chafya au kukuoa anaweza kuambukiza mtu mwingine. Pia, mtu yeyote akishika sehemu kwa mikono yake kama vile kiti cha gari, meza, kijiko, mlango, dirisha, kisha na wewe ukashika hapo unaambukizwa mara moja. Mdudu huyu inasemekana anao uwezo wa kukaa katika kiganja cha mtu kuanzia masaa 48 hadi 72.
Pia, anaambukizwa kupitia kukanya mkojo au kinyesi cha mwathirika.

D. DALILI ZA MTU MWENYE VIRUSI VYA KORONA.

1. Anakuwa na homa kama malaria
2. Anakuwa na kikohozi kikavu
3. Anakuwa na mafua na tabia ya kupiga chafya kila mara.
4. Anahisi maumivu kwenye miunganiko ya miguu yake(joints).
5. Dalili kubwa ni kupumua kwa shida kama mtu mwenye Nimonia.

E. TIBA NA CHANJO YA VIRUSI VYA KORONA.

Ugonjwa huu hadi sasa hauna tiba mbadala. Inasemekana wachina wamekuwa wakitumia madawa ya zamani yaliyowahi kutibu jamii.ya virusi kama hivi nyakati za nyuma ila mafanikio yake ni madogo.
Pia wachina inasemekana wanatumia ile dawa ya malaria ya zamani iliyojulikana kama CHROLOUINE ingawa nayo haina matokeo mazuri.
Pia, kuna dawa ijulikanayo kama KALETRA nayo inatumiwa kwa sasa japo haina matokeo mazuri kwa maana ilishindwa kutibu EBORA
Kuhusu chanjo bado haijapatikana isipokuwa Wamarekani wanaendelea kufanya utafiti kupitia wanyama kisha watafanya majaribio kwa wanadamu na tutaona matokeo yake.
Kwa upande wa chanjo

F. AMEKUWA NA ATHARI GANI TANGU AJE KWETU HUYU MDUDU?

Kutokana na taarifa tunazopata kupitia vyombo vya habari inasemekana hadi kufikia sasa idadi ya waathirika ni watu 80,000 duniani kote. Nchi inayoongoza ni china, inafuatwa na ITALIA kisha IRAN na nyinginezo. Hadi sasa ni nchi 40 zilizolipotiwa kuwa na ugonjwa huu.

E. JE KWELI WATU WANAELEWA HATARI YA HUYU MJAMAA AU WANAFANYA TU MIZAHA?

Nataka mjue kwamba tukifanya mizaa na huyu ndudu tutaisha. Mdudu huyu yuko katika kundi linaloitwa VIRUSI. Jamii ya wadudu walio katika hili kundi ni hatari kuliko OSAMA BIN LADEN, EL SHABAB, WATEKEBAN na HEZBOLLAH. Ogopa mdudu anayeitwa VIRUS. Yeye hana umbile maalumu, hubadilika badilika, pia, ni vigumu kufa kwa dawa. Labda umesahau! Ngoja nikukumbushe magonjwa yanayosababishwa na virusi ambayo hayana tiba mbadala hadi sasa. Unajua ugonjwa unaoitwa KANSA? UKIMWI?, EBOLA?!!!
Hupo mpaka hapo?? Sasa huyu jamaa anayeitwa KORONA ni yuko katika jamii hiyo hiyo ya AKINA UKIMWI. Tena nafuu ukimwi una dawa ya ARV ya kuongeza maisha, huyu mjamaa hadi sasa hana dawa rasmi. Ukimpata nafasi ya kuishi ni ndogo sana ndio maana unaona inanyonga hadi watu maarufu wenye pesa zao.

Huyu jamaa anaitwa KORONA ni hatari sana kwasababu anaambukizwa kwa hewa na kugusana. Wakati ukimwi unapatikana kwa ngono ya hiari, huyu jamaa anakwijia kwa kupenda kwako au kutopenda.

Fikiria ugonjwa huu ukija katika nchi maskini kama Tanzania au Kenya n.k tutaishi kweli??!!
Fikiria usafiri wetu wa MATATU na DALA DALA. Tutakufa wangapi?? Fikiria misongamano tuliyonayo sokoni, madukani, makanisani na misikitini? Fikiria juu ya watoto wetu mashuleni na vyuoni!! Nakwambia yanaweza kuwa mauaji au vifo vya ajabu!!
Ikiwa watu wanapata ugonjwa huu katika ndege vipi sisi tunaosafiri kwa mabasi na treini??!!

Hii ni mauti ya pili hakika!! Fikiria unaambiwa kwamba mwenye ugonjwa huo akishika kiti au meza nawe ukagusa hapo tayari anaingia kupitia viganja vyako. Na huyo mdudu anao uwezo wa kukaa kwenye mkono wako masaa 48 hadi 72. Je tutaenda wapi sisi maskini??!! Au tujufungie ndani??

Inasemekana ukimpata kwa mikono kisha ukajigusa kwenye pua au ndomo wako.tayari anaingia na baada ya week 2 dalili zinaanza.
Mtu mwenye hao wadudu unatakiwa uwe naye umbali wa mita mbili. Swali ni je utamjuaje?Wakati dalili zinaanza baada ya week au tatu tangu apate virusi hivyo?

Haya unaambiwa mwenye ugonjwa huo akipiga chafya au kukooa ukiwa karibu naye tayari umeisha. Unaambiwa ukikanya kinyesi au mkojo wa aliye na virusi tayari unao. Naona itakuwa kama mauaji ya Rwanda ya mwaka 1994.

Kusema ukweli iwapo tutaelewa hatari ya huu ugonjwa hatutafanya mizaa ninayoiona kwenye mitandao badala yake itatupasa kuomba Mungu na kuchukua hatua za kibinadamu.

F. HATUA ZINAZOSTAHILI KUCHUKULIWA KAMA KANISA DHIDI YA VIRUSI VYA KORONA.

Sisi kama kanisa wakati umefika lazima tuamke. Tusiachie tu serikali mzigo huu. Tutake tusitake inatulazimu sasa kuacha baadhi ya mila na taratibu zetu za kikanisa ambazo zaweza kusababisha maambukizi ya hawa wadudu.

Wakati umefika wa kuacha kusalimiana kwa mikono wakati wa ibada. Kwa wale wanaoshiriki meza ya Bwana kwa kutumia kikombe kimoja sasa nao.waache huo utaratibu. Wakati wa kuombea watu kwa kuwawekea mikono nao tuache. Sasa tuanze maombi ya bila kuweka mikono hadi.ugonjwa huu ukipata ufumbuzi. Pia, serikali ikikataza mikusanyiko ya kidini na kisiasa kama crusades na kadhalika pia tuwe watiifu kwa serikali inayotutakia mema sisi wananchi wake.

Najua wapo wachungaji, maaskofu, manabii na mitume ambao uenda wasikubaliane na mawazo yangu kwa kigezo kwamba sina imani.
Ni sawa tu waseme vile wataona ila wajue kuwa KUWA NA IMANI HAIMAANISHI KUWA TUSIWAJIBIKE. Ninachojua imani hai ni ile yenye matendo. Ndiyo maana Mungu aliahidi kutulinda lakini bado tunafunga milango yetu kwa kufuri. Ndiyo maana Mungu alisema yeye ni Mungu atuponyaye lakini bado tunaweka net ya mbu na kufyeka majani tusipatwe na malaria.

Pamoja na hayo, kama kanisa inapaswa tuanze naombi maalumu kwa ajili.ya kuombea nchi zetu na dunia kwa ujumla. Mungu ashindwi lolote anaweza kutusaidia maana dunia na vyote vilivyomo ameviumba yeye.

ONYO KWA WATU WOTE:
Huu siyo wakati wa kufanya mizaa dhidi ya huu ugonjwa. Tunatakiwa kufuata masharti ya afya. Mungu hashughuliki na wajinga ukijifanya eti una imani wewe haunawi mikono utakufa na utatuacha sisi tunaonawa mikono. Usife kwa ujinga kufa kwa mpango wa Mungu. Kila lililo jema hatuna budi kulifuata. Kuna mambo mengine Mungu ametupa akili kuyafanya bila maombi. Ukihisi njaa kula chakula na ukihisi kiu kunywa maji hakuna maombi ya kuondoa njaa wala kiu. Kuna sehemu lazima tuwajibike kama binadamu. Pamoja na maombi lazima kanuni za afya zifuatwe ama sivyo tutakufa kifo cha kijinga.

DUA YANGU DHIDI YA HUYU KORONA.

Naombea familia yangu na mimi mwenyewe na ndugu zangu na kanisa Mungu atuepushe na hili baraa kwa Jina la Yesu.
Naombea nchi yangu Tanzania na Kenya Mungu aiepushe ni hili baraa kwa Jina la Yesu.
Naombea nchi zote za jumuia ya Afrika Mashariki Mungu azirpushe na vifo kwa Jina la Yesu.
Naombea nchi zote za ulimwengu Mungu atuepushe na vifo vinavyoletwa na huyu KORONA kwa Jina la Yesu
Naomba asiwepo mtu yeyote aliye mshirika katika makanisa yetu wa kufa kwa Jina la Yesu.

NB: SHARE HUU UJUMBE UTABARIKIWA!
SHARE HUU UJUMBE KWENYE MAGROUPS YOTE YA WHATSAPP UNAYOJUA. SHARE KWA FACEBOOK NA COMMENT ILI TUELIMISHANE JUU YA KUSHINDA HUU UGONJWA KWA JINA LA YESU.

Imeandaliwa na BISHOP ASKOFU EDWIN ISRAEL MIHIGO.
INTERNATIONAL REVIVAL.CHURCH AFRICA, MWANZA, TANZANIA.
TEL. +254728535387 AU +255765545572

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad