Maalim Seif "Lowassa Alikuwa na Sababu za Kurudi CCM, Hakupata Alilotegemea"


Mwenyekiti wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad amesema yeye hawezi kumhukumu Lowassa kwa uamuzi wake wa kuondoka upinzani na kurudi CCM ingawa anakiri amewaumiza na kuwaangusha wapinzani kwa uamuzi wake huo

Amesema, Waziri Mkuu huyo wa zamani alikuwa na sababu nyingi za kumfanya arudi CCM ikiwa ni pamoja na msukumo wa familia lakini pia kutotendewa vema na chama hicho kikuu cha upinzani (CHADEMA)

Amefafanua kuwa Lowassa ni tofauti na yeye kwakuwa yeye ameweza kuvumilia mikikimikiki na matokeo ya kuwa mpinzani ila Lowassa alitoka kuwa Waziri Mkuu na kuna mambo aliyategemea Upinzani lakini hali ikawa tofauti na matarajio

Amenukuliwa akisema “Na ninavyosikia mimi familia yake ilimshinikiza, kwamba kuna mmoja kati ya wakwe zake alikuwa gerezani na watoto wake walikuwa wanamwambia ‘baba unaona… ndugu yetu sisi anapata shida kwa sababu wewe uko upinzani.’ Kwahiyo, lile shinikizo la familia lilikuwa kubwa sana"
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani huku CCM ndio alipata alichotaka?

    ReplyDelete
  2. Sefu unakumba siku ya ijumaa tulivyo kuwa Chimwaga na Marehemu Aboud na Mwalimu na nyiyi mpaka Idrisi akatokea.

    Ndio hicho hicho na Siasa ni kama ndoa yenye Talaka ikapita na kurudia. Mimmi sitoona ajabu hata wewe ukirudi tulipokulea to utotoni na kuku kuza.

    Wewe pia umepitia misuko suko mingi Afya na Umri unakwenda. Nassor Moyo ,Husni Makame. dkt Kingwaba wote wametutoka.


    Kaa Tfakari Jua nataa nini katika muda huu mchache uliobaki.

    waangaie wenzako Salim Ahmed, Ali Hassan, (Baba Rukhsa) hata mimi Baridi
    Malumbano si yetu tena..mwachie Heche na Lema sigara zao Misokoto. Rasta.

    Wewe unahitaji Heshhima yako. Sisi tunaitambua na hata Mh JPJM anatambua
    jitulize rudi nyumbani rekebisha mambo ukiwa ndani kwa muafaka sahihi ukijua JPM ni Msikivu na mpenda Haki. Bashiru pia kijana mwelewa.ni kijana mcha mungu mpenda watu, mtu wa watu.

    Maalim kaa jitathmini nini unahitaji kwa sasa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad