Maambukizi ya Virusi vya Corona Rwanda Yafikia Watu 50



Wizara ya afya nchini Rwanda imetanaza visa vipya 13 vya ugonjwa wa Covid-19 chini ya wiki mbili tangu mgonjwa wa kwanza kuripotiwa kuwa na ugonjwa huo na sasa idadi ya maambukizi kufikia 50.

Maambukizi ya sasa, watano walikuwa wametokea Dubai,mmoja ametokea Netherlands na mmoja ametokea Marekani na wote hao walikuwa karantini wakati walipowasili.

Huku wawili wameambukizwa wakiwa ndani ya nchi.

Rwanda imeweka vituo vitatu vya afya vya kupima maambukizi ya coronavirus, viwili viko Kigali na kingine kiko kusini mwa taifa hilo.

Wagonjwa wengi wa corona ambao wanatibiwa wanaonekana kupata nafuu, wizara ya afya imesema.

Mwanzoni mwa wiki hii, Rwanda ilitangaza kufunga mipaka yote ya nchi hiyo na watu kuamrishwa kusalia majumbani mwao katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.

Hatua zingine zilizochukuliwa ni pamoja na watumishi wote wa serikali na wa kibinafsi kufanyia kazi nyumbani na safari za kuenda mikoani kusitishwa kwa wiki mbili kukiwa na uwezekano wa muda huo kuongezwa.

Vilabu vya pombe na, maduka yasio ya chakula pia yamefungwa huku usafiri wa bodabobda ukisitishwa.

Hatua hiyo inajiri siku moja baada ya wizara ya afya ya Rwanda siku ya Jumamosi kutangaza kuwa watu wengine sita wameambukizwa virusi vya corona miongoni mwao mtoto mchanga wa miezi 10.

Maambukizi hayo yanaifanya Rwanda kuwa na idadi ya visa 17 vya maambukizi ya virusi vya corona.

Wananchi waliokuwa na hofu wameonekana wakinunua bidhaa za chakula huku baadhi yao wakihofia hali itakuaje.

Hatua zilizochukuliwa na Rwanda kudhibiti coronavirus ni kufungwa kwa shule zote za umma na za kibinafsi, maeneo ya kuabudu na sehemu zote za umma.

Matukio kama vile mikusanyiko ya watu katika maeneo ya michezo na harusini vimeahirishwa na wale waliopoteza wapendwa wao watazikwa kwa namna ya kipekee.

Shirikisho la Sola la Rwanda(FERWAFA), pia limetangaza kwamba michuano yote kwa sasa itafanyika bila kuhudhuriwa na mashabiki katika viwanja vya michezo, huku shirikisho la mpira wa mkono nchini humo likiahirisha michezo yake yote.

Maeneo ya umma na maeneo yote ya utoaji wa huduma yameagizwa kuweka vitakasa mikono kwa ajili ya umma unaotembelea maeneo hayo.

Raia wamehimizwa kukaa nyumbani na kuepuka matembezi yasiyo ya maaana na kunawa mikono mara kwa mara kwa muda wa sekunde 20.

Hakuna abiria atakayeruhusiwa kusimama na kutoa wito kwa watu wa eneo na vikosi vya usalama kusaidia kuhakikisha hatua hizo zinatekelezwa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad