Mahakama Kuu Tanzania..."Rais Anaweza Kushtakiwa Kwa Uvunjifu wa Katiba



Leo Machi 18, 2020, Mahakama Kuu Nchini imeeleza kuwa Rais wa Tanzania anaweza kushtakiwa kwa makosa ya uvunjaji wa Katiba

Jaji Lameck Mlacha wa Mahakama hiyo ametoa hukumu hiyo katika hukumu ndogo kwenye shauri lililofunguliwa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe dhidi ya Rais Magufuli

Zitto alifungua shauri Mahakamani hapo akidai Rais Magufuli alivunja Katiba baada ya kumteua Charles Kichere kuwa CAG akichukua nafasi ya Prof. Mussa Assad

Katika shauri hilo ambapo Zitto anadai CAG haondolewi kwenye nafasi hiyo mpaka astaafu, Serikali ilipeleka mapingamizi sita ambapo leo Mahakama imeyakataa. Shauri la msingi linaendelea
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad