Mzee Mangula Aanguka Ghafla na Kulazwa ICU.....Rais Magufuli Amjulia Hali



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo tarehe 29 Februari, 2020 amemtembelea na kumjulia hali Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndg. Philip Mangula ambaye amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.Ndg. Mangula aliugua ghafla jana na kisha kukimbizwa hospitali kwa matibabu.

Taarifa ya Mangula kuugua imetolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa huku video zikimuonyesha Magufuli akizungumza naye, baadaye kusali pamoja.

Mangula anaonekana akiwa amelala kitandani huku akiwa na plasta juu ya jicho lake la kushoto.

HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Mangula ambaye jana alishiriki kikao cha kamati kuu ya chama hicho sambamba na Magufuli kilichofanyika katika ofisi ndogo za CCM zilizopo mtaa wa Lumumba, Dar es Salaam, amelazwa katika chumba cha uangalizi maalum (ICU).

“Mangula aliugua ghafla jana na kisha kukimbizwa hospitali kwa matibabu,” inaeleza taarifa hiyo.

“Utapona na Mungu atakusimamia katika tatizo hili, sisi tulipoona jana umeanguka ilitushtua,” amesema Magufuli na Mangula kujibu, “sijui nimeangukaje.”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad