Marekani yaionya Iraq kuhusu mashambulizi dhidi ya kambi zake
Muungwana Blog · Muungwana Blog 2 · 12 hours ago
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo, ameionya Iraq akisema nchi yake italipiza kisasi ikiwa kambi za jeshi la Marekani zilizoko Iraq zitashambuliwa tena.
Katika mazungumzo ya simu na waziri mkuu wa Iraq Adel Abdel Mahdi, Tangazo la wizara ya mambo ya nje mjini Washington limesema kuwa Pompeo amesisitiza kuwa lazima wanaofanya mashambulizi dhidi ya kambi za Marekani wachukuliwe hatua.
Mazungumzo baina ya viongozi hao yalifanyika jana Jumapili, siku moja baada ya wanajeshi watatu wa Marekani kujeruhiwa katika shambulizi la maroketi dhidi ya kambi ya Marekani na washirika wake Kaskazini mwa mjini mkuu wa Iraq, Baghdad, likiwa la pili kubwa kuilenga kambi hiyo katika muda wa wiki moja.
Wanajeshi kadhaa wa Iraq pia walijeruhiwa katika shambulio hilo.