Web

Maskini Hizi Ndio Picha za Idriss Sultan Baada ya Kufikishwa Mahakamani..Tumuombee




Msanii wa vichekesho nchini, Idris Sultan na wenzake wawili wamefikishwa leo Machi 20,2020 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wakikabiliwa na kosa moja la kuchapisha maudhui mtandaoni bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Wakili Mushi amedai kuwa Idris na wenzake wametendeka kosa hilo kati ya Machi 8, 2016 na Machi 12, 2020 katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.

Imedaiwa katika maeneo hayo walirusha maudhui kupitia chaneli ya YouTube huku wakiwa hawana kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, washitakiwa wote walikana kutenda kosa hilo ambapo wakaachiwa kwa masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja kwa kila mshitakiwa ambao wamesaini bondi ya Sh.Milioni nane kila mmoja.

Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyi hadi Aprili 21,2020 ambapo itarudi kwa ajili ya kusikilizwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad