Mbabe wa zamani wa kivita DRC Germain Katanga aachiwa huru


Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Germain Katanga, aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka 12 katika mahakama ya kimataifa ICC, amechiliwa huru.

Hatua hii ya kumwacha huru Germain Katanga inakuja siku moja baada ya kuachwa huru kwa kiongozi mwingine wa waasi wa UPC Thomas Lubanga jijini Kinshasa nchini humo.

Taarifa ya kuachwa kwake huru imetolewa hapo jana na mpwa wake Jeannot Malivo Kagaba huko Kinshasa na kuthibitishwa mkuu wa shirika lisilokuwa la kiserikali linalotetea haki za wafungwa, Emmanuel Cole, na ambaye aliiambia AFP kuwa ni baada ya kukamilishwa kwa hatua zote za kisheria.

Katanga mwenye umri wa miaka 43, alihukumiwa kifungo cha miaka 12 Mwaka 2014 kwa kosa la kudhibiti uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu katika shambulio la kijiji huko Ituri, alihusika katika mauaji ya watu takriban 200 mnamo mwaka 2003 kaskazini mashariki mwa DRC

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad