Mbowe Asema Hawatalipiza Kisasi, Wataendelea Kuomba Umoja wa Kitaifa Mshikamano


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema amesema hawatalipa kisasi dhidi ya kichapo kilichotokea watakwenda kuomba umoja wa kitaifa mshikamano.

Mbowe aliyasema hayo jana usiku wakati alipomtembea hospitali Mbunge wa Bunda mjini, Ester Bulaya, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Jesca Kishoa ambao wamelazwa katika hospitali ya Agakhan baada ya kutembezewa kichapo juzi na askari magereza walipoenda kumpokea Mbowe gerezani.

“Hatutajenga wala kulipa kisasi mwenye kuhukumu ni mwenyezi Mungu na tutamuacha yeye, sisi tutaendelea kuomba umoja wa kitaifa, mshikamano wa kitaifa na msamaha kwa watu wote,” alisema Mbowe.

Aliongezea kuwa “Ninawashukuru Watanzania wote waluosimama upande wa haki leo nitazungumza na vyombo vya habari  kuwashukuru Watanzania kwa upendo wao waliotuonyesha usio na mipaka naahidi kusimama na watanzania wote,” alisema Mbowe.

Alisema wanahitaji kuwaona watu wote wawe salama na waione nchi yao ni sehemu salama  kwa kuishi.

Mbowe ambaye pia ni mbunge wa Hai, alisema watasimamia maadili yao na hawatajenga kisasi wala kulipa kisasi kwa sababu wana mambo mengi ya kufanya ya nchi na kesho yao kuliko kufikiria ya jana.

“Hatuwezi kufikiria nani amlipe nini wote ni wadhambi tunaangalia zaidi kuijenga kesho yenye matumaini kwa nchi kuliko kuitafuta jana yenye chuki na visasi kwa watu waliopo,” alisema Mbowe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad