Mbowe na Wenzake Waenda Gerezani Baada ya Kushindwa Kulipa Faini ya Sh Milioni 350
0
March 10, 2020
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake wamekwenda gerezani baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh 350 baada ya kuhukumiwa katika kesi iliyokuwa inawakabili ya uchochezi.
Leo viongozi hao nane wa Chadena na kada wa CCM Dk Vicent Mashinji wamehukumiwa kulipa faini ya jumla ya Sh milioni 350 ama kwenda jela miezi mitano baada ya kutiwa hatiani kwenye makosa 12 ikiwemo la kufanya maandamano.
Hukumu hiyo iliyochukua takribani saa 4, kuanzia saa 7 mchana hadi saa 11 jioni, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Thomas Simba baada ya kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka na ule wa utetezi.
Katika hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema amewatia hatiani washitakiwa katika mashitaka 12 kati ya 13, Kosa ambalo hawajatiwa nalo hatiani ni kosa la kwanza ambalo ni kufanya mkusanyiko usio halali.
Hakimu Simba amesema katika shtaka la pili la uchochezi lililokuwa likiwakabili watuhumiwa wote, kila mshtakiwa atatakiwa kulipa faini ya Tsh milioni 10 au kwenda jela miezi mitano.
Katika shtaka la 3 hadi 6, mahakama imeamuru kila mshtakiwa kulipa faini ya Tsh milioni 10 au jela miezi mitano.
Hata hivyo shtaka la 9, 10 linamhusu Mbowe peke yake, hivyo kila kosa atalipa Tsh milioni 5 au jela miezi mitano na katika shtaka la 11 atalipa faini ya Sh 10 milioni.
Katika adhabu ambayo, Mbowe amehukumiwa ni kulipa Sh.Mil 70, Halima Mdee Sh.Mil 40, Dr.Mashinji kulipa Sh.Mil 30, John Heche Sh.Mil 40, Msigwa Sh.Mil 40, Bulaya Sh.Mil 40, Mnyika Sh.Mil 30, Salum Mwalimu Sh.Mil 30 na Ester Matiko Sh.Mil30.
Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam
Tags