Mdau Aibuka Kuwafungukia Diamond na Harmonize "Hata Akiacha Mziki Leo Hakuna Wakuvunja Rekodi zake"


MDAU:"Ieleweke kwamba mimi Snitch mzuri mzuri ila niko mkweli. Nikianza na Album ya Harmonize ni mzuri kiasi chake yani haina maajabu sana kwa upande wangu. Ikumbukwe ni mimi sio wewe mimi huwa sio shabiki sana wa ngoma za Kiingereza nadhani ila pia Melody za Harmonize zimekuwa za kawaida sana.

"Sasa nirudi kwenye swala la Diamond Kupost.
Diamond kafanya poa sana Kupost ile kitu pale maana ake akata shombo. Yani pale anampunguza Harmonize taratibu na nina imani kibiashara pale Harmonize hajapenda

"Alafu swala la kusema kwanini hajapost kwenye page za Wcb Wasafi sio Facts kabisa. Page kubwa Tanzania hapa ni ya Diamond Platnumz. Yani page Yake ni zaidi ya TV stations. Sasa Kusema Mbona zingine hajapost sio. -
"Kingine ile ni Kampuni jamani sio personal, kwenye kampuni wanapost vitu vyenye Faida kwa kampuni. Albamu ya Harmonize haina faida kwenye kampuni ya Wcb_Wasafi. Sasa kwanini wapost jamani..?? DIAMOND kuzidiwa na Harmonize haitokaa itokee Milele mimi sio Mungu ila kutokea pia haiwezekani 😂😂🙆🙆.
"Ila uamini nikupe hii Ngoma kubwa kwa Harmonize toka atoke Wcb_Wasafi ni Uno, nenda Youtube imetazamwa mara ngapi?? Alafu Tazama Jeje ya Diamond mnayosema ina Beat ya Wizkid jumlisha matusi toa Mabwanga. Bado JEJE INA NGUVU kwahiyo kataa kubali Diamond kupinduliwa na wasanii wa Bongo haitokaa itokee hata akiacha muziki leo hakuna wa kuvunja Rekodi zake sahau. Cha mwisho H. BABA ndio mtu pekee anae faidika na Beef la Harmonize na Diamond

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad