Mfahamu Mwanamziki Nguli Brenda Fassie Kiundani zaidi


Kwa wale wahenga wenzangu je unazikumbuka nyimbo kama vile vulindela,  ngwanona, jiva, mama, thola, nakupenda,  na nyinginezo nyingi kutoka kwa mwanamziki Brenda Fassie.

 Kama  unazikumbuka nyimbo hizo basi naomba usome makala haya mpaka mwisho ili uweze kusoma historia ya mwanamziki huyo  kama ifutavyo:

Majina yake kamili anaitwa Brenda Nokuzola Fassie , alizaliwa Novemba 3, 1964 huko Langa Cape Town nchini Afrika Kusini, akiwa mtoto wa mwisho wa familia yenye watoto 8, jina la Brenda alilopewa lilitokana na wazazi wake kuwa mashabiki wa mwanamuziki wa Marekani Brenda Lee.

Baba yake alifariki akiwa na miaka miwili na kulelewa na mama yao pekee, ambaye alikuwa mcheza piano. Brenda alikuwa na kipaji tangu utotoni na kuanza kuimba na mama yake kwenye sehemu mbali mbali ambazo watalii walikuwa wanaenda.

Akiwa na miaka 16, Brenda Fassie tayari alikuwa na uwezo mkubwa wa kuimba na hata kuwa na bendi yake ya kitaa iliyoitwa 'The Tiny Tots'. Umaarufu wa Brenda ulianza kusambaa sehemu mbali mbali za Afrika Kusini na kumfikia producer wa muziki Koloi Lebona kutoka Johanesburg, na kuamua kwenda kwenye familia ya Fassie na kukutana na Brenda, na hatimaye kukubaliana kuondoka naye kwa ajili ya kuendelea na masomo na kufanya muziki Soweto.

Brenda akapata fursa nzuri ya kufanya kazi zake za muziki na kuwa maarufu zaidi. Alipomaliza mkataba na Lebona alianzisha bendi yake nyingine 'Brenda and the Big Dudes, na kurekodi hit song 'Weekend special' mnamo mwaka 1983, na kuwa rekodi iliyoongoza kwa mauzo Afrika Kusini, na kumpa ziara za kimuziki sehemu mbali mbali duniani.

Pamoja na bendi lakini Brenda alijiimarisha vizuri kama solo artist kwenye muziki wa Pop aliochanganya na mahadhi ya Afrika Kusini huku nyimbo zingine akiimba kwa lugha mbali mbali ikiwemo kingereza, Kiswahili, Kizulu na Xhosa.

Brenda alizidi kuachia kazi nzuri zilizofanya vizuri kwenye mauzo, nyimbo ambazo zilibeba jumbe mbali mbali kama za kupinga ubaguzi wa rangi, umoja, mapenzi na masuala ya kifamilia.

Maisha yake binafsi yakawa kwenye vyombo vya habari kama wasanii na watu wengine maarufu, mwaka 1989 aliolewa na Nhlanhla Mlambo na ndipo majanga yakaanza kumuandama, kwani mwaka uliofuata baada ya kuoana alishtakiwa kwa utapeli, na Agosti 1990 wawili hao waliachana.

Brenda alianza kutumia madawa ya kulevya pamoja na pombe kali na kuwa mlevi kupindukia, kitendo ambacho kilianza kumshusha kwenye kazi zake, huku wengine wakisema ndio mwisho wa 'Queen of Pop'. Skendo hazikuisha kumuandama kwani baada ya kuachana na mume wake alikumbwa na skendo chafu ya ngono ya kujihusisha kwenye mapenzi ya jinsia moja, na vyombo vya habari kuliweka kwenye 'front page'.

Matumizi ya madawa ya kulevya yalimuweka pabaya zaidi na mwaka 1995 kuamua kwenda 'sober house'. mwakaa uliofanya alifata 'comeback' ya nguvu huku akifanya kazi na mwanamuziki wa Congo ambaye ameshafariki Papa Wemba, na kuwa-prove wrong wale waliosema ameshaishiwa kwenye muziki, baada ya albam alizoachia kama 'Memeza' aliyoifanya na producer maarufu Afrika Kusini, Chicco, kufanya vizuri sokoni na kumpa tuzo kama Kora, SAMA na tuzo zingine za ndani.

Kitu ambacho wengi walikuwa hawajui baada ya kurudi kwenye game ni kwamba alikuwa akiendelea kutumia madawa ya kulevya, na mwezi April 2004 alikimbizwa hospitali baada ya kupata heart atack, iliyomplekea kuwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, na baada ya wiki alifariki dunia mnamo May 9, 2004.

Baada ya kifo chake madaktari waligundua madawa ya kulevya aliyokuwa akitumia ndio yalimletea tatizo la moyo, na zaidi aliyotumia usiku wa siku aliyokimbizwa hospitali, alitumia cocaine ambayo iichanganywa na sumu ya panya.

Nchi ya Afrika Kusini ilimpenda sana Brenda Fassie akiwemo aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Nelson Mandela, na alipofariki serikali ilitengeneza sanamu maalum iliyowekwa kwenye jumba la maonyesho kumuenzi mwanamuziki huyo wa Pop aliyetikisa Afrika na dunia, aliyepewa jina la 'Madonna of the township'.

Brenda alipofariki aliacha mtoto wa kiume aliyekuwa na miaka 19 anayeitwa Bongeni Fassie.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad