Mfanyakazi wa Facebook Apata CORONA Wafunga Ofisi Huku ikifunga Vyuo na Shule



Idadi ya watu waliofariki kutokana na #coronavirus Ulimwenguni imefikia 3,286, idadi ya Wagonjwa 95, 483 huku idadi ya Watu waliopona ikifikia 53,688. Ardhi Kuu ya China (Mainland China) pekee ina Wagonjwa 80,430 na vifo 3,013

Hadi napema leo, nje ya Ardhi Kuu ya China, vifo vingi vya ugonjwa huu vimetokea Italia kwenye vifo 107, Iran yenye vifo 92, Korea Kusini yenye vifo 35 na Marekani yenye vifo 11

Katika kuzuia kuenea zaidi kwa virusi hivyo, Italia imetangaza kufunga shule zote na vyuo vyote hadi Machi 15, 2020 huku Mtandao wa Facebook ukitangaza kufunga ofisi zake za Seattle kwa wiki moja baada ya Mfanyakazi mmoja kupata virusi hivyo

Aidha, watu 1,000 Jijini Yew York wameshauriwa kujiweka karantini huku Mamlaka zikiendelea kutafuta walioathirika. Shule ya Mount Vernon imefungwa hadi Machi 9 huku chuo cha ‘The Lake Washington Institute of Technology’ huko Washington nacho kikifungwa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad