Mke wangu Ananiambia Anatongozwa Sana, Nifanyeje?

Mke wangu amenishangaza sana baada ya kuniambia kuwa akiwa kazini au mizunguko huko mtaani kuwa anatongozwa sana na wanaume mbali mbali lakini eti anawakataa wote....

Maswali yangu
Wataalam wa mambo hivi Inapofikia hatua mke wako wandoa anakwambia hivyo ina maana gani?
Hivi Kweli Mwanamke anaweza kwa siku atongozwe na wanaume watano na kuwakataa wote?

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe na mkeo akili zetu siko sawa. Kwani kutongozwa kuna ubaya gani?? Wewe ulivyo mtongoza alikukataa au alikukubali. Kumbuka kutongozwa kwake kunatokana anavyo jionyesha mbele ya wanaumme, walegezee macho, watingishie matako, ongea kama kasuku, omba pesa, uliza maswali yasiokuwa na maana hapo na mambo mengine mengi utatongozwa tu na ikiwezekana utavuliwa chupi. Swali la mwisho mkeo anavaa pete au akisha ondoka nyumbani kwako anaiweka kwenye pochi. Kazi kwao hapa kazi tu.

    ReplyDelete
  2. Inawezekana na inaweza isiwezekane inategemea anajielewa vip na ww umekuwa mume wa aina gani kwake kama una kero na maudhi sahau kukataa akitongozwa atakubali ili ajipooze huko kutoka kwenye mikero yako na miudhi na migubu na mikoromo yako ya usiku na misoksi inayonuka yani list kero zako zooote anazovumilia...ila kama ni mume mwema unamjali unampenda una udhaifu tu wa kawaida wakuvumilika basi akitongozwa atakataa...

    ReplyDelete
  3. Akwambie na aliowakubalia

    ReplyDelete
  4. Anaposema nimewakataa wote inaonesha hakutokea anaempenda n pindi akitokea atakubaliana naye. Mwenye heshima anawezaaje kumwambia mume wa ndoa mambo hayo na pia huyo mume ana bwege la kutupa.onesha wazi kuwa

    ReplyDelete
  5. Kwanza hadi kutongozwa huoni kwamba yeye ndiye anayejilegeza ovyo. Mke anayethamini ndoa yake huwa hampi mwanaume mwingine nafasi ya kuongea zaidi ya salamu tu. Na usikute huwa anapenda kutongozwa na siku akimpata anayemuhitaji ndio utakoma. Elewa kwamba wewe sio type yake. Kwaheri kaka.

    ReplyDelete
  6. huyo hajielewi kama ange kua na jielewa asinge sena hinyo

    ReplyDelete
  7. YAANI WEWE MTOTO MOTO SANA HAYO MACHO YAKO TU YANAFANYA UTONGOZWA.LABDA TU UVAE MIWANI YENYE UFA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad