Mkutano Mkuu wa TLP kumpitisha Mgombea Urais Dkt. John Pombe Magufuli wa CCM.



Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimesema kuwa Mkutano mkuu wa chama hicho  utaofanyika Mei 9 mwaka huu Kitapitisha Mgombea wa Urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt.John Pombe Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Chama hicho Agustino Lyatonga Mrema amesema kuwa jina Mgombea Urais lilisgapitishwa na Halmashauri Kuu Chama na kilichobaki ni kudhibitisha jina la Mgombea huyo.

Amesema kuwa katika uchaguzi mkuu hakuna haja ya kuweka Mgombea wa Urais kutokana na Rais aliyopo amekidhi mahitaji ya watanzania.

"Hivi unasimamishaje Mgombea wakati Kazi aliyoifanya Rais aliyopo madarakani inaonekana,  kungewepo na tatizo ndio kungekuwepo umuhimu wa kusimamisha mgombea"amesema Mrema

Aidha Mrema amemshauri Mwenyekiti wa chama Cha NCCR Mageuzi James Mbatia kuutangazia umma kuwa Uchaguzi Mkuu utakuwa wa Uhuru na Haki pamoja na kuunga mkono juhudi za Rais aliopo madarakani.

Amesema Mbatia alishawahi kusema kuwa kusifu serikali ya iliyopo madarakani sio dhambi hivyo anaweza kuendelea kuunga mkono Rais wa Awamu ya Tano kuendelea kwa kipindi kingine.

Mrema amesema Rais Dkt.John Magufuli aachwe amalize malengo yake kuifikisha Tanzania anayoitaka ambayo ni Tanzania ya Maendeleo yanayoonekana.

Amesema TLP si chama cha kufuata upepo wa bendera bali ni chama kinachojua kinachofanyika na kuukubali uongozi ws Rais Dkt.John Pombe Magufuli.

Amesema vyama vingine vijifunze na kuangalia Rais Dkt.John Magufuli namna Tanzania iliyopata Maendeleo kw kipindi kifupi ikiwamo kukomesha Rushwa.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Swadakta Jogoo..!!!

    Yote uliosema ni sawa. TLP Kupeperusha mgombea wake baada ya Ridhaa ya Halmashaurri yake Si mwingine bali ni Kipezi chetu KI MAGU Chetu Orijino Jembe la MIsimu yote haina Kiagazi wala Masika au Vuli yuko mzigoni.

    Allah amlinde na amjaalie Afya,busara na Hekma aendelee kututumikia Inshaallah.

    ReplyDelete
  2. Swadakta Jogoo..!!!

    Yote uliosema ni sawa. TLP Kupeperusha mgombea wake baada ya Ridhaa ya Halmashaurri yake Si mwingine bali ni Kipezi chetu KI MAGU Chetu Orijino Jembe la Misimu yote haina Kiagazi wala Masika au Vuli yuko mzigoni.

    Allah amlinde na amjaalie Afya,busara na Hekma aendelee kututumikia Inshaallah.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad