Mtuhumiwa wa shambulizi dhidi ya waislamu katika mskiti nchini New Zealand akiri kosa mahakamani.
Mtu alieendesha shambulizi dhidi ya mskiti katika jimbo la Christchurch nchini New Zealand mwaka 2019 afikishwa mahakamani na kukiri kosa.
Brenton Tarrant alishambuliai mskiti na kuwaua watu 51 waliokuwa wakisubiri kufanya ibada Machi mwaka 2019.
Mshtakiwa huyo amekiri makosa yote aliosomewa na mahakama.
Waziri Mkuu Jacinda Ardern na jamii ya Waislamu nchini New Zealand wamefurahishwa na kitendo hicho, na hivyo kuruhusu mahakama kuendelea na kesi hiyo hasa kuchukua uamuzi dhidi ya Tarrant.
Muuaji huyo, mwenye umri wa miaka 29 amekiri makosa yanayomkabili bila kushinikizwa na mtu .