Munalove Atoa Tamko Zito Kuhusu Wanao Muhukumu Kuhusu Ulokole na Mavazi yake"


Munalove atoa tamko zito -

"Ninaomba mjue hili leo✍🏻.....Watu wengi mmekuwa mkinihukumu kwa hali tofauti pasipokujua kuwa mm nimeamua kumfuata Yesu Kristo kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu. Wengi mmenihukumu kwa mavazi, tembea ongea, hata baadhi ya vitendo ambavyo pia vingine havina uthibitisho lakin sasa elewa kuwa kwakuwa najua nilikotoka mpaka kufikia kuingia kwenye Wokovu. 
"Ninajua nitumie njia gani kuwafikishia wengine ujumbe ili kupitia mm nao wamjue Mungu ndo maana navaa kama wao, naongea Kama wao, natembea Kama wao . Lakini mimi si wao na hakika ashukuriwe Mungu kwakuwa sasa wapo ambao tayari wamemjua Mungu kupitia staili ya kufanana nao ili kuwafikishia Injili
"Hata Kama shetani akinipinga kupitia wanadamu sitaionea haya injili ya Kristo. Kwa kupitia mdomo wangu nitalisifu na kulitangaza Jina lake , Yeye aliyenitoa kwenye ubaya Ukabadilika kuwa baraka. Mbarikiwe endelea kuniombea nizidi kuitwa mshindi na Shetani atazidi kuaibika. AMEN

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad