Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr Harrison Mwakyembe, amesema ana tatizo la ugonjwa na msanii Harmonize kwa sababu kila anachokitoa kwake anakiona ni kizuri na anakifurahia.
Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe, kuli ni msanii Harmonize
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika uzinduzi wa album ya Harmonize iitwayo "Afro East" Dr Harrison Mwakyembe amesema Harmonize ni msanii bora ambaye ameleta mapinduzi, pia amewataka wasanii watunge nyimbo ya kutahadahrisha wananchi kuhusu ugonjwa wa Corona.
"Nimefurahi sana halafu nina tatizo moja la ugonjwa kwamba kila anachokitoa Harmonize ni kizuri na nakifurahia ndiyo maana ni mmoja wa wasanii bora hapa nchini, kumetokea mapinduzi makubwa ya kimuziki kwa miaka 10 iliyopita" amesema Dr Harrison Mwakyembe
Pia ameongeza kusema "Ila kinachoniuma tuna kumbi mbalimbali lakini hatuna ukumbi maalum kwa ajili ya muziki, ndiyo maana sisi tumeamua ndani ya wizara kuanzia mwezi Aprili tutaanza ujenzi wa ukumbi ambao utachukua watu elfu 50, 40, 30 kwa hapa Dar Es Salaam"