Aliyekuwa meneja wa Dogo Janja, Suma Mnazareti, Kitale, Sharomilionea pamoja na PNC amefunguka kwa kusema kwamba yeye aliwekeza zaidi ya tsh milioni 300 kwaajili ya kuwasaidia wasanii mbalimbali ambao walipita kwenye mikono yake.
Ostaz Juma na Musoma
Akizungumza na Bongo5 wiki hii baada ya ukimya kwenye game kwa muda mrefu, Ostaz amedai pesa hiyo ambayo aliiwekeza kwenye muziki wake haikuwahi kurudi huku akidai katika wasanii ambao alionja pesa zake ni Kitale pekee.
Ostaz Juma ambaye kwa sasa maisha yake ameyaelekeza kwenye kusoma dini akiwa na mtoto wake wa kwanza.
“Muziki unahitaji wawekezaji, mimi niliwekeza kwenye muziki zaidi ya tsh milioni 300 na hata mia sikupata. Nakumbuka pesa ambayo niliionja ni kutoka kwa msanii ni tsh laki nane kutoka kwa msanii wa muziki na filamu Kitale na pesa hiyo sikumuomba yeye tu aliamua kunitumia baada ya kupiga dili” alisema Ostaz.
Aliongeza, “Kuna wasanii wengine unaweza kuwasimamia kwenye muziki na wasitoke, sometimes unaweza kuhisi wana mikosi, hata ukitumia njia gani hakuna kitu kitakwenda. Lakini namshukuru Mungu wale wachache ambao niliwasaidia waliweza kufanya vizuri na kubadili maisha yao kwa sababu mimi mara nyingi nilikuwa sitegei kwamba nitapata chochote bali nilikuwa nawasaidia tu”
Ostaz Juma kwa sasa amesema anaona muziki umekuwa lakini bado kuna changamoto ya wasanii wachache ambao wanafanya vizuri ambapo amewataka wadau wa muziki kuwashika wasanii wote na sio kuchagua wasanii wakuwa-support