Povu.! Wastara Kumgombania Z Anto kwa Binti Kiziwi


Moja kati ya stori ambayo inazungumziwa kwa sasa ni juu ya mahusiano kati ya msanii wa filamu Wastara Juma na Z Anto, ambapo watu wengi hawakutegemea kama wawili hao kama wangekuwa wapenzi.

Mahusiano yao yame-trend  zaidi  baada ya Wastara kumtishia kumchana viwembe mke wa zamani wa Z Anto, ambaye ni Binti Kiziwi kuwa aache kumtafuta mwanaume wake, hali iliyopelekea kuonekana wanamgombania mwanaume mmoja.

Kupitia EATV & EA Radio Digital, imempata Wastara Juma na amenyoosha maelezo kuhusu tukio zima la kumgombania Z Anto ambapo amesema.

"Nimetoa onyo mtu asimsogelee Z Anto kutoka sebuleni hadi chumbani, kwahiyo nimeweka kizuizi, nimemshambulia Binti Kiziwi kwa sababu ndiye aliyenifanya nimshambulie na wengine wajue kabisa wakija kumgusa wawe wamejipanga maana tutatoana macho"  amesema Wastara Juma.

Aidha ameongeza kusema  "Kumgombania ni suna kwa sababu nina wivu, ukiona mwanaume namgombania ujue ananiridhisha kwa kila kitu, mwanamke ambaye anaridhishwa na aliyepitia kwenye  mahusiano hawezi kukubali kumpoteza mtu wake".

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mfunge kwamba umzuie akitoka nje sio wa binti kiziwi tu kaa ulijue hilo leave z anyo alone katafute mizee ziwe yako

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad