Raia 13 wa China wazuiwa kuingia Kenya wakitokea Tanzania
0
March 19, 2020
Kenya. Watu 16 walizuiwa kuingia nchini Kenya kupitia mpaka wa Lunga Lunga katika mji wa Kwale wakitokea Tanzania
Kati ya watu hao, 13 ni raia wa China.
Raia hao wa China ni Xiao Zhanquan, Xu Shaul, Xu Duo, Lyu Xiaohua, Zhou Changyong, Jiang Chunyang, Xiao Zhanquan, Lyu Xiaohua, Wang Xiaoba, Shang Deyuan, Huang Honghui, Yang Yubiao na Cao Bingwang.
Watu hao walisindikizwa na madereva watatu wa Tanzania ambao ni Saidi Seif Mapunda, Hassan Mohammed Makolo na Wema Ramadhani Muambeya.
Ripoti ya Polisi iliyoonwa na kituo cha runinga cha Citizen Kenya inaonyesha watu hao waliwaambia wakaguzi katika eneo hilo kuwa walikuwa wanaelekea mjini Mombasa kwa ajili ya kazi maalumu katika kampuni ya Bamburi Cement Ltd.
Hata hivyo, baada ya mahojiano zaidi ilitakambulika kuwa tangu walipowasili nchini Tanzania kati ya Machi 4- 16, 2020 hawakutimiza siku 14 za kujitenga katika karantini zilizowekwa kwa ajili ya kujikinga na virusi vya corona.
Wote 16 walizuiwa kuingia Kenya kutokana na kutokidhi maagizo ya kujikinga na kuzuia kuenea kwa virusi vya corona na walirudishwa mpakani.
Tags