Ronaldinho na Kaka yake Wadakwa kwa Kukutwa na hati Bandia ya Kusafiria


Nyota wa zamani wa soka wa Brazil, Ronaldinho na kaka yake wamekamatwa wakituhumiwa kutumia hati bandia za kusafiria kuingia nchini Paraguay, mamlaka zimesema.

"Ronaldinho atahojiwa saa 2:00 asubuhi leo Alhamisi katika ofisi ya mwendesha mashtaka," Waziri wa Mambo ya Ndani, Euclides Acevedo aliwaambia waandishi wa habari.

Polisi wa Paraguay walivamia hoteli jijini Asuncion ambako mshindi huyo wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia ya mwaka 2005 alikuwa akiishi akiwa safari yake ya kutangaza kitabu, na wakakuta nyaraka hizo za kughushi, waziri huyo alisema.


"Pia tunachunguza uwajibikaji wa mamlaka zilizomruhusu kuingia nchini kwa kutumia hati feki za kusafiria," alisema Acevedo.
HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Ronaldinho na kaka yake walipokonywa hati zao za kusafiria Novemba mwaka 2018 baada ya kushindwa kulipa faini ya dola 2.8 milioni (sawa na Zaidi ya Sh5 bilioni za Kitanzania) kwa kuharibu mazingira, kosa walilofanya wakati wa ujenzi wa nyumba jijini Rio Grande do Sul, kusini mwa Brazil.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad