Samatta aipa neno Man City, fainali Carabao Cup


Mshambuliaji wa Aston Villa, Mbwana Samatta ataweka historia nyingine hii leo kuwa mtanzania wa kwanza kucheza fainali ya Carabao Cup katika uwanja wa Wembley nchini Uingereza.

Aston Villa itavaana na Manchester City, huku Samatta akitarajiwa kuwa ndiye mshambuliaji tegemeo wa Aston Villa akiwa amefunga bao moja katika michezo mitatu aliyoichezea timu hiyo.

Kuelekea mchezo huo, Samatta amesemakuwa anajisikia mwenye bahati kubwa kwani amecheza mechi mbili tu na amefanikiwa kuingia fainali, "maandalizi ya mchezo huu ni makubwa na ninaona kabisa kuanzia kwenye mazoezi kuwa tunakabiliana na changamoto kubwa, nasi tumejiandaa kwenye mchezo huu".

"Ni habari njema sana kwangu, nimejiunga na klabu na baada ya mechi mbili tu ninacheza fainali. Ni wakati mzuri sana kwangu", ameongeza Samatta.
HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Mara ya mwisho kwa Aston Villa kushinda taji ni mwaka 1996, iliposhinda kombe la ligi kwa kuifunga Leeds United. Inakutana na Manchester City ambayo ni bingwa mtetezi wa kombe la Carabao huku kocha wa Man City, Pep Guardiola akiwa na rekodi nzuri kuelekea fainali hiyo kwani mpaka sasa amecheza jumla ya fainali 24, akishinda 20 na kupoteza fainali nne pekee.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad