Senegal na Tunisia zimethibitisha kuwa na waathirika wa corona.
Waziri wa afya wa Senegal Bw. Abdoulaye Diouf Sarr amesema mgonjwa aliyeambukiziwa ni raia wa Ufaransa, baba wa watoto wawili, alirudi Dakar mnamo tarehe 26 mwezi Februari kutoka Paris kwa ndege ya Senegal, baada ya safari ya mapumziko kusini mwa Ufaransa.
Tarehe 28 mwezi Februari, idara ya afya ya Ufaransa iliarifiwa na zahanati binafsi kuwa mtu mmoja alionyesha dalili za COVID-19, baadaye alithibitishwa kuambukizwa COVID-19 katika Taasisi ya Pasteur mjini Dakar, lakini hali yake sio mbaya, na familia yake imewekwa kwenye karantini.
Waziri huyo amewataka raia wasichanganyikiwe, na kuchukua hatua za kujikinga zinazotangazwa na wizara ya afya.
Mgonjwa aliyebainika Tunisia ni Raia wa Tunisia ambaye ametokea Italy.
Nchi zenye Watu wenye virusi hivyo kwa Afrika zimefikia tano, nyingine ni Algeria,Misri na Nigeria