Senegal: Waliobainika Kuwa na Corona Wafikia Wanne

 
NCHI ya Senegal hapo jana imeripoti kesi mbili mpya za maambukizi ya virusi vya Corona nchini humo, Miongoni mwa watu walioambikizwa virusi hivyo ni pamoja na mwanamke wa mmoja wa wagonjwa wanaoendelea kuhudumiwa, ambaye anaishi nchini Ufaransa.

Mgonjwa mwingine ni raia wa Uingereza, ambaye alitoka London wiki moja iliyopita. Wote wawili wamewekwa karantini katika Hospitali ya Fann.

Jumatano hii, vipimo vilivyofanywa na taasisi moja nchini Senegal, Institut Pasteur, vinaonyesha kuwa mwanamke wa miaka 68 pamoja na mumewe wa miaka 80, ambao walikuwa wamekuja kuhudhuria mazishi ya mpendwa wao huko Guédiawaye wamepatikana na virusi vya ugonjwa hatari wa Covid-19.

Uchunguzi ulifanyika papo hapo ili kujaribu kupata watu waliokuwa nao karibu. Serikali ya Senegal imewataka raia kutoa ushirikikiano wao katika kukabiliana na kuenea kwa ugonjwa huo unaotia wasiwasi dunia.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad