Serikali :Hatujakosa FEDHA ya Kujenga SGR, Wanaobeza Miradi Wapuuzwe



Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema Serikali haijawahi kukwama kwa namna yoyote ile kifedha katika utekelezaji wa ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) na kuongeza kuwa, treni hiyo itaanza rasmi kazi mwaka huu

Dkt. Abbasi ameeleza kuwa, ujenzi wa Dar - Morogoro umefikia 75% na ule wa Morogoro - Makutupora umefikia 28% huku sehemu kubwa ya ujenzi wa Dar - Morogoro imetandazwa reli na kuwekewa nyaya za umeme

Msemaji huyo amesema ujenzi wa SGR umegharimu Tsh. 2.957 Trilioni hadi sasa, na zaidi ya Trilioni 7 zitakatumika kukamilisha ujenzi huo

Amesema madai ya baadhi Wanasiasa kuwa Serikali haina fedha kwa ajili ya kujenga Reli hiyo hayana ukweli wowote na kutoa wito kwa Wananchi kupuuza uzushi huo

HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Amewataka wanaokosoa miradi ya Serikali kufanya hivyo kwa haki badala ya kuongea uongo kwani Tanzania ni Nchi ya Demokrasia
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa wazaiaji, tusipo wapenyua na kuwarudisha makwao Uvira.
    wataendelea kuchonganisha watanzania naserikai yetu.

    Haitakii mema nchi hii. amefunga safari kujaribu kuiharibia Tazania mikop ya Elimu n kashindwa lakkini alijaribu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad