Zoezi la kunyunyizia dawa ya kuua vijidudu katika katika maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi Jiji la Dar es salaam limeneendelea usiku wa kuamkia leo Machi 31 katika standi kuu ya mabasi ya Ubungo na mitaa yake ikiwa ni moja ya jitihada za Serikali kukabiliana na virusi vya Corona ambavyo ni tishio kwa dunia kwa sasa.
Dk. Fodi Chisongela, Mratibu wa zoezi zoezi la unyiziaji dawa kwa ajili ya kuua wadudu wadhurifu na vimelea vya magonjwa mbali mbali ikiwemo Corona amesema awali, walipuliza Ilala, na Kinondoni na sasa wapo Ubungo na wanatoa kipaumbele kwa kituo cha mabasi cha ubungo kwani kinatembelewa na watu wengi.
“Tumekuja na magari matatu ikiwemo pickup ikiwa na pamp maalum ya kuua wadudu wazurifu, gari la zimamoto lenye uwezo wa kubeba lita za maji elfu 18 ambazo zimewekwa na gari la polisi la kutuliza ghasia,” Amesema.
Ameyataja maeneo mengine lengwa kwa upulizwaji dawa usiku wa jana kuwa ni barabara ya HSekilango yote mpaka Bamaga, Mwenge, Mlimani City, Survey, Chuo Kikuu na kutokea mataa ya Ubungo.
Naye Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ubungo, Dk. Peter Nsanya alisema, hatua zinazofanyika ni katika utekelezaji wa maagizo ya Mh. Paul Makonda ambaye aliagiza waue vidudu vyote vinavyosababisha magonjwa mbali mbali ikiwemo Corona.