Shirika La Afya Duniani Lashauri Kuepika Matumizi ya Noti....



Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshauri kutumia pesa zisizohusisha kushika kwa kuwa noti zinasambaza #Coronavirus. Shirika la Afya limeonya kuwa Kirusi cha #COVID19 kinaweza kubebwa kwenye noti kwa siku nyingi

Ili kuzuia maambukizi ya #coronavirus watu wanaweza kutumia pesa isiyohitaji kushikwa inapowezekana, kama kulipa kwa kadi au Pesa za mtandao, pia kuosha mikono yao wakishika noti

Benki ya Uingereza pia imetambua kuwa noti zinaweza kubeba bakteria au virusi na wameshauri kunawa mikono mara kwa mara. Mwezi uliopita, China na Korea walianza kuzitibu noti zao kama njia ya kuzuia maambukizi ya #Coronavirus

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad