AZAM FC jana Machi 4, 2020 imeshindwa kufuta uteja wake wa msimu wa 2019/20 mbele ya Simba kwa kukubali kichapo cha mabao 3-2 Uwanja wa Taifa.
Kwenye mchezo wa kwanza ambao uliwakutanisha Simba na Azam, matajiri hao walipoteza kwa kufungwa bao 1-0 na mfungaji alikuwa ni Meddie Kagere na jana Machi 4 walikubali kudufugwa mabao 3-2 huku Kagere akiwatungua pia bao moja la ushindi.
Ushindi wa Simba unawafanya wajikite kileleni wakiwa na pointi 68 baada ya kucheza mechi 26 huku wakiwaacha Azam FC nafasi ya pili wakiwa na pointi zao 48.
Machi 8, Simba itakuwa na kibarua cha kumenyana na Yanga mchezo utakaochezwa Uwanja wa Taifa huku wakiwa na kumbukumbu ya kutoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 mchezo wa kwanza.
Sven Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa atawaandaa vijana wake kwa umakini.