Web

Tamko la Maaskofu wa Anglikana Kuhusu Corona



P.O. Box 899, Dodoma, Tanzania

Tel: +255 (0) 262321437/2324574

Fax: +255 (0) 262324565 

Email: act@anglican.or.tz 

Archbishop: The Most Rev. Maimbo William Fabian Mndolwa, General Secretary: The Rev. Can. 

Mecka Ogunde. 

19 Machi, 2020 

 

TAMKO LA MAASKOFU WA KANISA ANGLIKANA TANZANIA KUHUSU TAHADHARI YA UGONJWA WA VIRUSI VYA CORONA (CORONAVIRUS AU “COVID -19”) 

Wapendwa Katika Kristo, Bwana Yesu Asifiwe, 

Tarehe 17 Machi, 2020, Serikali yetu kupitia Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ilitangaza rasmi kuwepo kwa ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na virusi vya Corona (Coronavirus au “COVID -19”) ulioanzia nchini China mwezi Disemba mwaka 2019 na kuenea sehemu mbalimbali hapa Duniani. 
Serikali imebainisha hatua mbalimbali ambazo imechukua na zinazoendelea kuchukuliwa ili kukabiliana na ugonjwa huo hapa nchini. 
Kwa kuzingatia mwongozo na maelekezo hayo ya Serikali, sisi Maaskofu wa Kanisa Anglikana Tanzania kama viongozi wa Kiroho wa Kanisa, tunatoa tamko hili ili lisomwe kwa wakristo waliomo kwenye Dayosisi zetu zote ishirini na nane (28) na kwa wananchi wote. 
Kupitia Tamko hili, tunaendelea kuunga mkono jitihada zote zinazofanywa na Serikali yetu katika kukabiliana na ugonjwa huu wa Corona (“Covid -19”) nasi sasa, tunawahimiza wakristo wote kudumu katika sala na maombi ili Mwenyezi Mungu ambaye ni mwingi wa rehema alinusuru Taifa letu na maradhi haya. Sala zetu zifanyike katika ngazi mbalimbali za Kanisa, Jumuiya na familia. Tunaishauri serikali kuhimiza vyombo vya usafiri kuchukua hatua za tahadhari, mfano kusafisha mabasi, ndege na maeneo ya usafiri. Kanisa linaiomba serikali kusimamia mfumko wa bei za bidhaa muhimu kama vile sanitizers na vyakula katika kipindi hiki cha mlipuko wa korona. 
Neno la Mungu linasema: 

“Nikizifunga mbingu isiwe mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwapelekea watu wangu tauni; ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao. Sasa macho yangu yatafumbuka, na masikio yangu yatasikiliza maombi ya watu waombao mahali hapa (2 Mambo ya Nyakati 7:13-15) 

Sisi Kanisa, tunayo imani kubwa sana kuwa, hakuna lisilowezekana kwa Mungu. Hivyo, kwa kuwa ugonjwa huu umetangazwa katika kupindi hiki cha Kwaresima ambapo tupo katika majira ya toba na kufunga kuelekea Pasaka, tunahitaji sana kuendelea kupiga magoti na kujinyenyekeza mbele za Mungu kwa maombi ya kuutafuta uso wa Mungu huku tukiziacha njia zetu mbaya. BWANA ambaye ni mwingi wa rehema atasikia sala zetu na kuturehemu. 
Kanisa linaelekeza kwamba, kila Dayosisi itenge siku maalumu ya maombi kuanzia leo tarehe 19 Machi, 2020. Aidha, kwa pamoja kama Kanisa, tunatanganza kuwa, siku ya Ijumaa Kuu itakuwa ni siku ya Ibada ya pamoja ya Kanisa Anglikana Tanzania kuombea Taifa letu dhidi ya ugonjwa huu wa corona. 
Kwa wale walioathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na ugonjwa huu wa corona, sisi kama Kanisa, tunasimama nao katika maombi na pia tunaendelea kuwahimiza Watanzania wote kwa umoja wetu na kwa imani yetu, tuendelee kumwomba Mungu kusudi aweze kuliepusha Taifa letu na athari za ugonjwa huu wa Corona pamoja na changamoto nyingine za kijamii na kiuchumi zinazoihusu nchi yetu ili Mungu atunusuru na kutuvusha salama. 
Tutaendelea pia kuwaombea na kuwatia moyo wafanyakazi wote ambao wanahusika katika maeneo mbalimbali ya kukabiliana na ugonjwa huu wakiwemo madaktari, wauguzi, watoa huduma za afya na nyinginezo, viongozi wetu wa juu wa Serikali ili Mungu aliye mwingi wa rehema aweze kuwalinda na kuwaongezea ujasiri zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao katika kipindi hiki. 
Tunawahimiza na kuwataka wakristo wote kuendelea kuchukua tahadhari juu ya ugojwa huu wa Corona kwa kuzingatia maelezo ya Serikali yenye lengo la kujikinga na kuwakinga wengine na ugonjwa huu hatari. Pamoja na hatua hizi, Kanisa linahimiza Dayosisi zote na Wakristo wote wa Kanisa Anglikana Tanzania kutekeleza yafuatayo ili kupunguza athari za kuenea kwa virusi vya Corona katika maeneo yetu: 

3(i) Kupunguza mikusanyiko isiyo ya lazima katika maeneo yetu. Na pale inapolazimu kukutana, tujihimize wakristo wote kujitenga kwa umbali ulioshauriwa na Serikali ili kuepuka kukaribiana na kuongeza mazingira ya athari za maambukizi. 

(ii) Tujitahidi kutoa taarifa kwenye mamlaka husika mara tunapobaini kuwepo kwa dalili za maambukizi ya ugonjwa huu kama zilivyobainishwa na Serikali ambazo ni pamoja na homa, kikohozi, ugumu wa kupumua au upungufu wa pumzi, maumivu ya kudumu au shinikizo kwenye kifua. 

(iii) Kuepuka kusalimiana kwa kushikana mikono na kujitahidi kusafisha mikono yetu mara kwa mara kwa sabuni au sanitizer kwa kuzingatia ushauri wa Wizara ya Afya tuwapo mahali pa umma au tunapokohoa, kushika usoni au kupiga chafya. 

(iv) Tunahimiza milango na madirisha ya Makanisa kuachwa wazi wakati wa huduma na ibada ya umma ili kuwezesha hewa kuingia. 

(v) Kuhusu wagojwa, tunahimiza wahudumiwe kwa maombi ya mbali, kwa kuzingatia njia zinazoruhusu mikusanyiko ili kuepusha maambukizi zaidi. Tunaamini kuwa, kwa Mungu, hakuna umbali katika maombi. 

(vi) Makanisa yawe na maeneo ya kunawia mikono yenye sabuni na maji yanayotiririka ili watu waweze kunawa mikono kabla ya kuingia na baada ya kutoka Makanisani. 

Mwisho, tunafahamu athari za ungojwa huu na tunahitaji kuwa waangalifu sana. Hata hivyo, hatupaswi kuishi kwa hofu kuu kiasi cha kushindwa hata kufanya ibada zenye tahadhari kama Wakristo. Sambamba na tahadhari zinazoshauriwa, tuendelee kumwamini Mungu yeye yupo na hivyo tudumu sana katika maombi ili aweze kutunusuru na janga hili. Tukumbuke kuwa Mungu ni mwenye rehema nyingi na ataturehemu. 

TAMKO HILI LIMETOLEWA NASI, hapa Jijini Arusha katika Kikao cha Nyumba ya Maaskofu, leo tarehe Kumi na Tisa katika mwaka wa Bwana wetu Yesu Kristo Elfu Mbili na Ishirini. 

tanahsanía 

1. The Most. Rt. Rev. Maimbo William Fabian Mndolwa, Tanzania na Tanga, 
2. Rt. Rev. Sadock Makaya, Western Tanganyika 
3. Rt. Rev. Dr. Jacob Chimeledya, Mpwapwa 
Rt. Rev. Dr. Dickson DaudChilongani, Central Tanganyika 
Rt. Rev. Dr. Elias Chakupewa, Tabora 

Rt. Rev. Isaiah Chambala, Kiteto 

Rt. Rev. Dr. Michael Hafidh, Zanzibar 

8. Rt. Rev. Godfrey Mbelwa, Lweru 
9. Rt. Rev. Mathew Mhagama, South West Tanganyika 
10. Rt. Rev. Dr. Stanley Hotay, Mount Kilimanjaro 
11. Rt. Rev. Julius Lugendo, Southern High Lands 
12. Rt. Rev. Dr. Joseph Mgomi, Ruaha 
13. Rt. Rev. Dr. Sospeterndenza, Kibondo 
14. Rt. Rev. Oscar Mnung‘a, Newala 
15. Rt. Rev. Dr. Given Gaula, Kondoa 
16. Rt. Rev. Godfrey Sehaba, Morogoro 
17. Rt. Rev. Raphael Haule, Ruvuma 
18. Rt. Rev. Dr. George Okoth, Mara 
19. Rt. Rev. Vithalis Yusuph, Dioceses of Biharamulo 
20. Rt. Rev. Dr. Mwita Akiri, Tarime 
21. Rt. Rev. MathayoKasagara, Lake Rukwa 
22. Rt. Rev. Jackson Sosthenes, Dar es Salaam 
23. Rt. Rev. John Lupaa, Rift Valley 
24. Rt. Rev. Dr.James Almasi, Masasi 
25. Rt. Dr. John Adiema, Rorya 
26. Rt. Rev. DalingtonBendankeha, Kagera 
27. Rt. Rev. Johnson Japheth Chinyong‘ole, Shinyanga 
OPEN IN BROWSER

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad