Tathmini Kuhusu Uzinduzi wa Albamu ya #AFROEAST ya Harmonize



March 14, 2020 tulishuhudia Mkali Konde Boy, Tembo, Mmachinga wa zamani Harmonize akiweka historia ya kuzindua Albamu kibabe ya AfroEast na haya ni maoni yangu.

Kiukweli tangu nipate akili ya kufuatilia masuala ya burudani, Jumamosi niliona uzinduzi wa level ya juu sana na kibabe kama wote hapa nchini

STEJI/ JUKWAA

Kwanza tuanzie hapa steji haikua ya kitoto nadhani ni kutokana na mchango wa bosi kubwa Majizo kuingilia kati suala kama alivyoeleza Konde Boy mwenyewe kupitia joto la asubuhi kwa Gerald Hando.

Ile steji haikuwa ya kawaida. Ilikuwa imewekewa muda maalum, ukifika huo wakati inajifunga, na kwa host alikua limited na muda wa kuuliza maswali na Konde Boy kujibu, steji ilipojifunga na seti zilibadilishwa kwa ajili ya ngoma nyingine.

Steji na Sound ilikua safi kama inavyokuaga kwenye matamasha ya Mkuu Majizo.

MUUNGANIKO WAWATANGAZAJI/ COOPERATES/ WASANII

Moja ya creativity kubwa ambayo niliikubali sana ni pale tu ambapo kulikua na watu maalum waliokuwa wakitambulisha nyimbo ambazo Harmonize alikua akienda kuziimba.

Pale tulishuhudia Wakurugenzi wa Kampuni / Wasanii na Watangazaji wakitambulisha ngoma iliyokua kwenye Albamu then Konde Boy anaiimba baada ya hapo alipata nafasi ya kumuuliza maswali Konde Boy ambayo ilikua content kubwa sana kwa Blogs, website na Mitandao ambayo kazi yao kutoa taarifa.

Kwa Cooperates kama Sayona unaona kabisa alitendewa haki kwa sababu kuna wakati Konde Boy aliwapa mention moja kubwa na kibabe kabla hajajibu swali, hakika pale nadhani Sayona alifurahi sana.

Kuuliza swali kwa Bosi swali Multichoice Nataka Shelukindo pale kuli-secure endorsment nyingine yano mfanyabiashara muaminifu ukiingia naye makubaliano na anaweza kukupa Bonus kwenye mkataba mliosaini (Safi Sana).

Kwa watangazaji uliona jinsi walivyogawanywa; walikua wa maeneo mbalimbali Ile ilijibu kile ambacho nilikiandika miezi michache iliyopita (Tathmini yangu kwa Harmonize nje ya WCB) kuwa angehitaji kurejesha mahusiano na media ambalo kwa lile tukio amefanikiwa kwa asilimia 200

Moja ya vitu vingine ambavyo niliviinjoy sana ni pale kuona viongozi wa kisiasa, wakijumuika na wasanii, wafanyabiashara kuhakikisha Albamu ya #AfroEast ya Konde Boy inakua kubwa zaidi.

Mwanzoni nilihisi tukio lingekua la kawaida kama ambavyo wasanii wengine huwa wanafanya Ila nilipokuja kuona Kiongozi Mstaafu wa Nchi anaamua kuacha usingizi wake na kwenda kwenye uzinduzi ndipo nikasema hili tukio si la kawaida linaenda kutikisa nchi, kiukweli uwepo wa Baba Jakaya Kikwete ilileta msisimuko mkubwa sana hata kwa watu wasiopenda burudani.

Uwepo wa viongozi wa Serikali na Chama ulionesha unabaraka za watu wote kilichobakia ni kupendwa Tu na Watanzania ambacho ndicho kipo sasa.

NYIMBO ZA ALBAMU

Kuanzia nyimbo ya 1 - 18 zote ni Fire Ila ukiniuliza mimi naipenda ni ile 'Fall in Love' na 'Mama' ngoma kali kwangu kuanzia utunzi mpaka beat.

MPOKI NA SHILOLE

Kama wanavyosema hata jambo jema sometimes huwa halikosagi kasoro, kwangu changamoto ndogo ambayo niliiona ni matumizi ya lugha kwa baadhi ya Stars wetu mfano Mpoki kuna wakati alilazimisha kutumia maneno ambayo nadhani hakujua kuwa kulikua na Watanzania wengine wanatazama na pale alikuwepo Mkuu wa nchi Mstaafu the same kwa Dadangu Shishi (Tuwasamehe)

All in All tusubirie tuone je ni kweli Album hailipi kama inavyodaiwa na baadhi ya Wakongwe nchini

By Sangu J

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad