Tausi Amjibu Wema Sepetu "Imemshtua Sana, Awe Mvumilivu"



Muigizaji Tausi Mdegela amesema, taarifa za yeye kujifungua mtoto zimemshtua staa wa filamu Wema Sepetu kwa sababu hakutegemea, na ujauzito wake alikuwa anauficha sana tofauti na watu wengine walivyozoea.


Msanii huyo wa filamu amesema hivyo baada ya kusambaa kwa taarifa zinazosema, Wema Sepetu alitokwa na machozi baada ya kusikia Tausi amejifungua salama mtoto wa kike.

"Inawezekana Wema Sepetu ananipenda sana, pia imemshtua kwa sababu nimeficha sana mimba yangu kwa muda mrefu tofauti na ingekuwa kila siku watu wanajua kwamba nina ujauzito na nitajifungua, na atakuwa ameshtuka kwanini nimeamua kufanya hivi au kuwa na mtoto" amesema Tausi Mdegela.
HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Aidha Tausi Mdegela amemwambia Wema Sepetu awe mvumilivu kwani wapo wanawake wengine ambao walipata watoto wakiwa na umri mkubwa, pia asiache kumuomba Mungu na aamini kile anachokifanya na Mungu atamsaidia.

Pia ameongeza kusema alikuwa hataki kupata mtoto, wakati akiwa na umri mdogo kwa sababu alikuwa anahofia akili yake bado haijakomaa na atashindwa kumlea mtoto.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad