TRA yawajia Juu Kampuni Ambazo Hazilipi Kodi


Na Thabit Madai, Zanzibar.

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema itaanza mpango wa kuzitoza kodi baadhi ya makampuni ambazo hazilipi kodi kwa kisingizio cha kupata hasara katika biashara zao.

Hayo ameyasema Afisa Mwandamizi wa Huduma na Elimu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa upande wa Zanzibar Shuweikha Salum Khalfani huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo wakati akiwasilisha mada ya taarifa za Mapato  ambayo imewashirkisha watembezaji watalii.

Amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji kodi kwa baadhi ya makampuni kutolipa kodi kwa kisingizio cha kupata hasara kwa biashara zao.

Aidha  amesema kuwa ulipaji wa  kodi hiyo utakuwa ni asilimia 0.5 ya mauzo ya mwaka kwa makampuni ambayo yamepata hasara kwa miaka mitatu mfululizo.

Pia amesema sheria ya mapato ya 2004 imeeleza kuwa kodi ya mapato ya biashara au uwekezaji itatathiminiwa na inapaswa kulipwa kila mwaka wa mapato kwa mtu binafsi  au kampuni.

“ Sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015 imemtaka mtu yoyote anayefanya uwekezaji au biashara ajisajili TRA na kupatiwa utambulisho wa mlipa kodi ndani ya siku 15 baada ya kuanza biashara au uwekezaji”amesema afisa muandamizi huduma na elimu.
Vilevile Afisa huyo ameelezea kuwa tafiti nyingi duniani zinaonesha kuwa Serikali mapato yake yanatokana na ulipaji kodi na sio wahisani wala mikopo.

 Amesema kuwa Serikali hutumia kodi kwa kugharamia huduma mbalimbali zinazotolewa kwa jamii kama vile ulinzi,elimu,afya na miundo mbinu.

Nao washiriki wa semina hiyo wameiomba Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kuunda sherian itayowabana wale ambao wanatembeza watalii bila ya kulipa kodi .J

Aidha wamesema Serikali inategemea zaidi mapato kutoka sekta ya utalii lakini kumekuwepo na baadhi ya watembezaji watalii hawalipii kodi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad