Tukio Llililotokea Mwezi Uliopita Linanithibitishia kuwa "Binadamu Wote ni Sawa ila Hatupo Sawasawa"


Mwezi uliopita majira ya saa 9 usiku zilisikika kelele kutoka kwa majirani wakisema "mwizi, mwizi"

Japokua nilisikia hizo kelele lakini sikutaka kutoka nje moja kwa moja kwasababu ni risk sometimes na hii nimejifunza baada ya tukio baya lililomtokea ndugu yangu.

Wakati niko ndani nikasikia sauti nje ikitokea kwenye ile nyumba iliyokua ikipiga kelele za kuita mwizi kuwa "aah wana bahati wamekimbia siku nyingine watakuja kufa kijinga"

baadhi ya majirani waliamshwa na ile sauti na ikabidi kuwauliza waliokua wanaita mwizi nini kimetokea. "Kuna wezi walikua dirishani wanataka kuiba na ndio maana tumeita mwizi"

Basi mimi niliposikia hivyo nikaona haina sababu ya mimi kutoka nje kama mwizi kasepa na hakuna alichoiba so ikanibidi niuchape usingizi tu.

Kesho yake tena majira ya saa 10 na robo usiku nyumba ile ile tena nikasikia kelele za kuita mwizi. Round hii nikachomoka na kinondo flani hivi huwa nakiweka nyuma ya mlango nikafungua geti ili niweze kukabiliana na huyo mwizi.

Katika hali isiyo ya kutarajia nikaona yule aliyeitwa mwizi anakuja kwangu na wakati huo mimi nipo getini bado sijafunga hata geti.

Huyo aliyekuwa akiitwa mwizi alikimbia na kuingia getini kwangu huku mimi nikiwa nimeduwaa. Kivipi mwizi akimbilie ndani mwangu wakati humu si sehemu salama kwake yeye wakati akijua kua itawarahisishia wananchi kumpiga kwa uraisi kwa sababu hatakua na sehemu ya kukimbilia.

Ikabidi nimfuate lakini nilishtushwa na sauti yake "Scars wananiua bure mi sio mwizi"

Nikataharuki kwa mshangao mkubwa kwasababu sauti hiyo ilikuwa si ngeni masikioni mwangu. Hapo ndipo nilipomsogelea kwa ukaribu na nikapata kujua kuwa yule ni mshkaji wangu wa kitaani.

Wakati huo alikuwa amelala chini huku damu zikimvuja kama maji, aah nilidata nikajikuta namuuliza maswali ambayo yalikuwa yananitatiza "daah mwanangu imekuaje umekuwa mwizi na mtaani wote wanakujua kuwa wewe ni fundi"?

Jamaa alijibu kwa shida sana maneno yake yalisikika kwa mbali kama mtu anayeweweseka, "Scars nilipigiwa simu kuwa kuna kazi inabidi nikaifanye na ndo maana nimejihimu asubuhi ili kuepukana na foleni maana kazi naenda kufanyia mbali. Lakini nilipofika hapa nashangaa wamenivamia na kunichoma visu kuwa mimi ni mwizi japokuwa niliwaambia kuwa mimi ni kijana wa mtaa huu huu"

Hapo nikaona niwaite vijana makamo yangu tusaidiane kumbeba mshkaji kumpeleka hospitali

Tulivyokua tunamnyanyua pale chini ndipo tulipobaini kuwa jamaa kashambuliwa vibaya sana. Shingoni kulikuwa na kitobo ambacho kilikuwa kinavuja damu ambazo zilimfanya akose nguvu ya kusimama peke yake.

Tukamchukua mpaka dispensary ya mtaani hapa ili aweze kupata matibabu ya huduma ya kwanza lakini wauguzi hawa hawakumhudumia chochote ndugu yetu wakatuambia tumpeleke Amana huku tukifuatilia PF3.

Tukakodi bajaji fasta fasta tukampakia huku akiongozana na kaka yake kuelekea hospitali ya Amana. Huku mimi nikirudi home kusafisha mazingira ya pale maana damu ilitapakaa ndani kiasi cha kufanya paonekane kama ni Vingunguti.

Majira ya saa 4 asubuhi tuliletewa taarifa kua jamaa kashafariki na ukweli halisi ni kwamba jamaa kauliwa kimakosa. Waliyemdhania kuwa ni mwizi alikimbia na walipotoka kumkimbiza wakakutana na huyu mshkaji wetu ambaye alikuwa mpita njia tu asiye na hatia akielekea kazini. Aisee nilihuzunika sana siku hiyo.

Hata kama angekua mwizi kweli Japokuwa wanasema huwezi kuthubutu kumpiga mwizi kama hukuwahi kuibiwa. Lakini hapana sio kwa kiwango cha kufikia kumpiga visu vya shingoni binadamu mwenzako bila huruma.

HIZI HABARI KAMA HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL BLOG <DOWNLOAD HAPA>

Halafu bora hata wagemkuta anavidhibiti kuwa ni yeye kafanya, maskini hata yule mwizi halisi aliyekimbia naye hakufanikisha kuiba chochote.

Wapumbavu wachache walikuwa wakisema siku yake ilifika

It's Scars

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad